Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Mwariko amewataka wakuu wa idara na vitengo kuacha upendeleo wakati wakufanya mapendekezo ya wafanyakazi mahiri na kuachana na tabia ya kupeana zamu.
Ameyasema hayo wakati anaongea na wakuu hao Ofisi kwake ambapo amewaeleza uzoefu unaonyesha kwasasa ipo tabia ya upendeleo au upangaji wa zamu za kuchagua mfanyazi bora kwenye idara na vitengo pasipo kuangalia uhalisia wa umahiri wa mtu katika utendaji kazi.
Mkurugenzi Mwariko amesema hali hiyo inawavunja moyo wale wanaojituma katika kutekeleza majukumu yao na kusababisha mdondoko wa ufanyaji kazi kwa inaondoa hali ya kujituma kwa wale wenye bidii kazini na wazembe kuona hakuna sababu ya kubadilika.
“Haipendezi na haina maana kama kuna watu watakua wanajituma katika kufanya kazi na unapofika muda wa kupongeza kwenye utendaji watu munapanga zamu ya kupeana zawadi hii inavunja moyo wa mfanyakazi kujituma lakini pia inaduma huduma zinazotolewa katika taasisi tafadhali tusinye hivyo”. Alieleza Mkurugenzi
Baadi ya Wakuu wa idara waliochangia jambo hilo wamepokea ushauri huo kama jibu sahihi la kuinua hari ya kujituma kwa watumishi katika majukumu yao ya kila siku nan i matarajio yao kuwa sasa kila mmoja ataona thamani ya kazi inayoifanya tofauti na hapo awali.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa