Mkuu wa wilaya Newala Mh. Mwangi Rajabu Kundya amewataka wananchi kujiandaa na zoezi la sensa ya watu na makazi 2022 kwa kuwa na taarifa sahihi za kaya zao kabla ya zoezi zipatikane takwimu za kweli.
Ameyazungumza hayo jana 18/05/2022 katika kikao cha kamati ya sensa ya wialaya cha utoaji elimu kwa maafisa watendaji wa kata wa halmashauri ya mji Newala kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mhe. Kundya amewasisitiza watendaji wa kata kutoa elimu kwa wakuu wa kaya na familia kuwa na taarifa sahihi za watu wao ili kurahisha zoezi la sensa, jambo ambalo litapelekea kutimiza lengo mahususi la serikali la kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya amewataka watendaji wa kata kushirikiana na madiwani katika kutoa elimu huku akiwaomba kubainisha changamoto na viashiria vyote vinavyoweza kujitokeza na kuathiri zoezi hilo ili kamati ya wilaya iweze kuzipatia ufumbuzi mapema.
Naye mratibu wa sensa halmshauri ya mji Newala Ndg. Simplis Frank amesema ili zoezi la sensa lifanikiwe ni lazima wananchi wapate uelewa wakutosha juu ya umuhimu wa kushiriki kuhesabiwa pamoja na manufaa yatokananyo na zoezi hilo.
Aidha amebainisha kuwa kamati ya maandalizi ya sensa ya wilaya imeazimia elimu ya sensa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao vyote vya kiserikali kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji, kata, halmashauri hadi wilaya kwa lengo la kujenga uelewa wa kutosha kwa wananchi.
Akiongea kwa niaba ya madiwani Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaeni ni diwani wa kata ya Nanguruwe Mhe. Yusuph Kateule amesema wao kama madiwani watasimama mstari wa mbele katika kuwafikia wananchi kuwapa elimu jambo la msingi kwao ni kujengewa uelewa wakutosha.
Zoezi la sensa ya watu na makazi nchini linatarajia kufanyika mwezi wa nane kwa wananchi wote kuhesabiwa kila mmoja pale alipolala kuankia siku ya sensa Tarehe 23/08/2022.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa