Mkuu wa wilaya ya Newala Alhaji Rajabu Kundya amewataka wananchi wa Newala kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kulinda afya njema zao na kuondokana na madhara mabaya yanayoweza kujitokeza kwa kutochanja ikiwa pamoja na kifo pale unapotokea mlipuko wa maambukizi.
Kundya ameyasema hayo Alhamisi 28/07/2022 kwenye viwanja vya kituo cha mabasi Newala mjini, wakati anaongea na wananchi waliojitokeza kwenye tamasha la kampeni ya Mziki Mnene iliyoandaliwa na Wizara ya afya chini ya usimamizi wa EPIDEMIC CONTOL (FHI 360) na EFM kwa ajili ya kuhamasisha kuchanja na kudhibiti maambukizi.
Amesema watu wenye kujali afya zao duniani kote tayari wameshachanja chanjo ya UVIKO-19 kwa kuzingatia kuwa kumekuwa na mabadiliko ya wimbi la maambukizi ya ugonjwa huo hivyo usalama na njia pekee ya kujiepusha na athari za UVIKO ni kupata chanjo na ndio maana hata viongozi wa serikali kuanzia Rais wetu wa Tanzania Mama Samia Suluhu, mawaziri na viongozi wengine wameshachanja.
“kuchanja.. tuwe na afya njema.. wajanja duniani kote wameshachanja, usipochanja likitokea wimbi la uviko tutakufa kama kuku wenye mdondo.. kuepuka balaa hilo tuchanje, Rais.. Rais Mama Samia Suhulu Hassan amechanja, waziri wa afya amechanja, mimi mkuu wa wilaya nimechanja, wajanja wote wamechanja wewe je.?” amesisitiza Mkuu wa Wilaya.
Akiongea katika tamasha hilo wakatia anamkaribisha mkuu wa wilaya kaimu Mkurugenzi amabaye pia ni Afisa Sheria wa Halmshauri ya Mji Newala Ndg. Deogratius Kaijage amesena halmashauri inahitaji nguvu kazi imara kufanikisha shughuli za maendeleo za kuijenga Newala hivyo kila mmoja anapaswa kujali afya yake kwa kuchukua hatua ya kujikinga na uviko kwa kuchanja.
Naye Mganaga mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Joseph Fwoma amesema lengo la tamasha hilo linalosimamiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau EFM na FHI 360, ni kuhamasisha watu kuchanja kwa kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja wapate chanjo, ugonjwa wa Korona upo na una sababisha vifo kwa hasa wasio na kinga na kinga yake ni kupata chanjo ya UVIKO-19.
Kampeni hiyo ya kuhamasisha kuchanja chanjo ya UVIKO-19 ilikwenda sambamba na tamasha hilo limepewa jina la Mziki Mnene na kubeba kauli mbiu ya Ujanja Ni Kuchanja lilijumuisha burudani ya muziki kutoka wasanii maarufu nchini pamoja na waigizaji kama Mkojani, Wema Sepetu, Man Fongo na wengine wengi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa