Mkuu wa wilaya Newala mhe. Aziza Mangosongo leo 15/10/2019 amefungua mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata, Vijiji na Mitaa wa halmashauri ya mji Newala na kuwataka kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi kama miongozo ya kisheria inavyoelekeza.
Mhe. Mangosongo amewataka wasimamizi hao wasadizi kutambua dhamana waliyopewa kuwa ni kubwa hivyo vitendo vyovyote watakavyofanya kinyume na taratibu za uchaguzi ni uvunjifu wa sheria hivyo hatua zitachukuliwa kwani kila mmoja ameapa kutii kanuni na taratibu.
Hata hivyo amewasisitiza kujiepusha na mitego ya wanasiasa ambao kwa kipindi kama hiki wamekua wakitafuta urafiki na uswahiba kwa maslahi yao binafsi ya kisisasa na wanaweza kuwa chanzo cha kuvuruga uchaguzi na kusababisha dosari mbalimbali hatimae kuitia hasara serikali.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya amewakata wananchi wa Newala wenye sifa ya kugombea na kupiga kura kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi na kujiandikisha katika maeneo wanayoishi sambamba na kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi.
Zoezi la kuandikisha wapiga kura litaanza jumanne tarehe 08/10/2019 na kumalizika tarehe 14/10/2019 ambapo kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia 18 na akili timamu atatakiwa kujiandisha kwenye daftari la mpiga kura katika mtaa au kitongoji anachoishi na uchaguzi utafanyika tarehe 24/11/2019.
Picha Zaidi..
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa