Afisa elimu ya awali na msingi Halmashauri ya Mji Newala Mwl. Sylivia Mutasingwa amesema watahiniwa 2516 kutoka shule 48 za msingi wanatarajia kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2025.
Mwl. Mutasingwa ameeleza kuwa kati ya watahiniwa hao, 1264 ni wavulana na wasichana 1252 huku shule za mfumo wa kiswahili ni 47 na shule 1 binafsi ni ya kiingereza ambapo kwa ujumla maandalizi yake yamekamilika.
Aidha katika kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri amewaomba wazazi kushirikiana na walimu kuwandaa watoto kiakili, kuwapatia vifaa na mahitaji ya darasani pamoja na chakula
“walimu wameshafanya kazi ya kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya mtihani na watoto nao wamesema wapo tayari hivyo niwaombe wazazi nao watoe ushirikiano kuwapa hasaha, chakula na vifaa vitakavyotumika wakiwa kwenye mtihani”
Afisa huyo amesema ni matarajio yao kuona wanaongeza ufaulu wa 85% walioupata mwaka jana huku akiwaonya wasimamizi kuepuka kuwasaidia watahiniwa na kuepuka udanganyifu aina yoyote wawaache watoto watumie maarifa waliyopata kujibu mtihani.
Kwa upande wake mwalimu wa taaluma katika shule ya msingi Lindumbe Mwl. Warioba Marwa ameeleza kuwa wamefanya maandalizi mazuri kwa kufanya mitihani ya moko mkoa, wilaya pamoja na mitani ya ndani na ujirani mwema.
Baadhi ya wanafunzi wanaotajia kufanya mtihani huo Shakuu Rashidi pamoja na Nadia Shaibu wa shule ya msingi Lidumbe wameahidi kufanya vizuri huku wakiwa na matarajio ya kufika mbali kielimu.
Mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa mwaka 2025 utafanyika kwa siku mbili, utaanza Jumatano Septemba 10 na kuhitimishwa Alhamisi Septemba 11.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa