Watanzania wametakiwa kuuheshimu na kuunga mkono muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa mataifa yenye nguvu duniani ni yale yaliyounganisha nchi mbalimbali.
Wito huo umetolewa leo Jumanne Apili 26, 2022 na Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Mwangi Rajabu Kundya katika sherehe za maadhimisho ya siku ya muungano wa Tanzania bara na visiwani iliyoadhimishwa kiwilaya katika hospitali ya halmashauri ya mji Newala.
Mhe. Kundya amesema taifa lililotokana na muungano wa nchi ndilo lenye uchumi imara, nguvu yakidola na maamuzi na kwa muungano wa Tanzania unao faida nyingi za uchumi na usalama unaochochewa na waasisi wake ambao waliweka mbele maslahi ya watanzania katika mkataba wa kuunganisha nchi hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Daudi Mwariko amesema ni muhimu kuuenzi muungano huu wenye thamani kamili ya Nchi yetu kutokana misingi na malengo madhubuti ambayo yaliwekwa na waasisi wake.
Aidha amefafanua kuwa kutokana na umuhimu wa siku yenyewe halmashauri iliamua kuadhimisha kwa kufanya usafi eneo la hospitali ya wilaya, kutoa vipimo bure vya magonjwa wasiyopewa kipaumbele kwa wananchi pamoja na kutembelea na kuwasadia wazazi katika wodi ya Watoto.
Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Newala Dkt. Mohamedi Khalifa amesema unaona faida kubwa ya muungano na yeye mwenyewe ni mfano wa matunda ya muungano japokuwa amezaliwa visiwani lakini ameajira Tanzania bara pasipo kuwa na vikwazo vya ukabila na utaifa.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa