• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Newala Town Council
Newala Town Council

Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano ya Umma
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi, Maliasili na Mipango Miji
      • Kazi
      • Usafi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Video
    • Maktaba ya picha

Kamati ya lishe mnalo jukumu kubwa la kuisaidia jamii kuhusu lishe

Posted on: July 24th, 2020

Wajumbe wa kamati ya lishe halamshauri ya mji Newala wametakiwa kutambua wanalo jukumu kubwa la kuisaidia jamii ipate uelewa wa kutosha ili iondokane na matatizo ya watoto kupata utapiamlo, udumavu, mgongo wazi na wajawazito kupata kinga wakati wa kujifungua.

Hayo yameelezwa Jumatano Julai 22,2020 na Mwenyekiti wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Bw. Kalistus Komba cha kikao robo ya nne 2019/2020 ambapo amewasisitiza wajumbe kushirikiana kutoa elimu jamii kwa kuwa lishe ni eneo nyeti linalochangia ustawi wa Taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara inayotokana afya bora.

Afisa Lishe wa halamashauri hiyo Ndg. Enos Kuzenza amesema halamshauri imeendelea kupata mafanikio katika kugawa vidonge vya FEFO kwa wajawazito na kufikia 85% ambapo kwa robo ya tatu ilikua 80% na utoajia elimu ya unasihi wa ulishaji kwa wazazi wenye watoto miezi 0-23 kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii (CHWs) umefikia 22% kutoka 5% robo iliyopita ambapo watu 1136 wamepatiwa elimu ambapo waliotaraji.

Aidha ameyataja mafanikio mengine kuwa ni kuvuka malengo na kufikia 117% ya kutoa elimu ya uhanisi kwa wazazi na walezi wenye watoto wa miezi 0-23 kutoka kwa watoa huduma za afya ngazi za vituo vya kutolea huduma (HWS) ambapo wazazi 9286 walipata elimu wakati matarajio yalikua 5260 na hiyo imetokana na watoa huduma wa vituo vyote 16 vya halmashauri walipatiwa mafunzo tofauti na robo iliyopita ambayo ni watoa huduma wa vituo vitatu ndio walipatiwa mafunzo.

Kuhusu utapiamlo amebainisha kuwa watoto 21 waliochini ya miaka 5 walibainika kuwa na utapiamlo mkali, 16 kati yao walitibiwa hospitali na kupona na wengine 5 wanaendelea na matibabu nje ya hospitali.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri Dkt. Athanase Emmanuel ameitaka jamii kuachana na mazoea hasa katika matumizi ya chunvi isiyo na madini joto hasa ya mawe ambayo wananchi wengi wanaikimbilia kutokana na urahisi wa bei, na kuagiza kila muuzaji wa chumvi ya mawe ni lazima awe na kibali cha halmashauri ambacho atakipata baada ya chunvi yake kupimwa kiwango cha madini joto na atakaebainika kwenda kinyume atakuchuliwa hatua kali.

Naye Afisa Afya wa halmashauri Bi. Zainabu Iddi ameiomba jamii kuachana na dhana potofu ya kuwazuia wajawazito kutumia vidonge vya FEFO kwa madai kwamba watapata matatizo wakati wa kujifungua jambo ambalo ni upotoshaji na inapelekea kumfanya mama mjamzito na mtoto anayetarajiwa kuwa kwenye hatari kupoteza maisha wakati wakujifungua au mtoto kupata ulemavu.

Wajumbe wa kamati hiyo wamesema wapo tayari kwa pamoja kushirikiana na wataalamu kwenda kwenye jamii kutoa elimu kwa kuwa suala la lishe linaonekana halipewi kipaumbele na wananchi wa kawaida kutokana na kutotambaua athari zinazojitokeza.



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2020 November 22, 2020
  • USAILI MTENDAJI WA KIJIJI July 24, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA April 22, 2020
  • TANGAZO NAFASI 1 YA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI III LINARUDIWA July 10, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAS MTWARA: Madiwani halmashauri ya Mji Newala wasilisheni hoja za wananchi

    December 04, 2020
  • Kamati ya lishe mnalo jukumu kubwa la kuisaidia jamii kuhusu lishe

    July 24, 2020
  • Halmashauri ya mji Newala yapenga matundu 240 ya vyoo, kampeni ya shule ni choo

    July 17, 2020
  • Newala Day yaweka mikakati wa kuondoa sifuri kidato cha nne na cha pili

    July 15, 2020
  • Tazama zote

Video

Mapokezi ya mwenge wa uhuru Halmashauri ya Mji Newala
Video nyingine

Kurasa za Haraka

  • Sanitation day
  • Tender
  • Uhuru torch

Kurasa Mashuhuri

  • Higher Education Students' Loans Board
  • National Examinations Council of Tanzania
  • Tanzania National Electoral Commission
  • PSPF Pension Fund
  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration and Local Government

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Newala-Mtwara

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 39

    Simu: (+255) 023 2935398

    Mobile: PS (0684439199)

    Barua pepe: info@newalatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Disclaimer
    • Sera ya Faragha
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya eneo la tukio
    • Huduma

Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa