Wananchi 757 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti na shinikizo la damu katika kampeni ya siku 5 iliyoendeshwa na taasisi ya kudhibiti saratani ya matiti JHPIEGO chini ya ufadhili wa Pfizer foundation wakishirikiana na halmashauri ya Mji Newala.
Bi. Hadija Shakila afisa muuguzi msaidizi na mtakwimu wa saratani ya matiti halmashauri ya Mji Newala ameeleza kuwa watu wa jinsi zote walijitokeza na kati yao wanaume walikuwa 59 na wanawake 698 huku 76 miongoni mwao walibainika kuwa na dalili za awali.
Afisa huyo amesema “katika hao 76 sio kama wameshajulikana wana saratani hapana, hao ndio tumeona wana dalili moja au mbili yakuashiria ugonjwa wa saratani. baadaya kurudi vipimo ndiyo tutajua wapi ambao wana shida na ambao hawana shida.”
Kapande wake Dkt. Rashid Suleiman mtaalam mbobezi wa upasuaji na mratibu wa kampeni hiyo amebainisha shida ya magonjwa ya matiti ikiwemo saratani ya matiti nchini ni kubwa ikihusisha na wanaume ambapo 1% hadi 5% ya wanaume wanaugua saratani ya matiti.
Mkurugenzi wa taasisi ya kudhibiti saratani ya matiti JHPIEGO Dkt. Maryrose Giattas amesema taasisi yake inafanya kazi katika mikoa minne ya Tanzania bara Mwanza, Tanga, Morogoro na Mtwara wakilenga kupunguza ukubwa wa tatizo.
Dkt. Maryrose amefafanua sababu za kuchagua mkoa wa Mtwara “kulingana na takwimu tulizonazo mkoa una wagonjwa wengi wa saratani mbalimbali sio tu ya matiti tulishirikiana wizara ya afya kuchakata data na kwa mkoa wa Mtwara tunasaidia halmashauri zote tisa”.
Aidha ameeleza kuwa katika kutekeleza jukumu la mradi huo la kudhibiti saratani ya matiti nchini JHPIEGO inashirikiana na wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wasimamizi wa afya ngazi ya mkoa na halmashauri chini ya ufadhili wa Pfizer foundation.
Kampeni ya uchunguzi saratani ya matiti halmashauri ya Mji Newala ilianza tarehe 05/08/2025 na kuhitimishwa tarehe 09/08/2025 ikiendeshwa kwenye vituo vitatu vya zahanati ya Makonga, kituo cha afya Mkunya pamoja na hospitali ya wilaya ya Newala.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa