Ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Maguful ya ujenzi wa barabara ya Mnivata, Nanyamba, Tandahimba, Newala mpaka Masasi wenye urefu wa kilometa 160 pamoja na daraja la Mwiti mkoani Mtwara, ipo mbioni kutekelezwa huku wananchi wakitakiwa kutumia fursa za ajira zitakazo jitokeza.
Hayo yameelezwa mjini Newala Jumatano Mei 20, 2020 na Ofisa Sayansi ya Jamii Mkuu wa wakala wa barabara Nchini (TANROADS) makao makuu ndg. Gibson Mwaya, wakati wa kikao cha Tanroads na madiwani, wakuu wa taasisi, watendaji wa Kata pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya mji Newala, cha kuelezea hatua za utekelezaji wa mradi huo.
Mwaya amesema uzoefu unaonyesha wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo miradi ya maendeleo inatekelezwa hawajitokezi kwenye kuomba kazi hata sizizo na taaluma maalum, badala huwapisha wageni kutumia fursa hiyo na wao kuwa watazaji hivyo amewataka wawakilishi hao kuwaelimisha wananchi kuwa hiyo ni fursa ya ajira na maendeleo.
Aidha amewaka wananchi kutambua kuwa maendeleo yoyote yana hasara ndani yake hivyo amewataka kuwa makini na muingiliano na wageni watakao kuja wakati wa utekelezaji hasa katika kujikinga magonjwa ya maambukizi ya zinaa kama UKIMWI, mimba zisizotarajiwa, uvunjivu wa ndoa pamoja na mambo mengine ya anasa na starehe.
Aidha amempongeza Mhe. Rais kwa kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha na Bank ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) imeonyesha nia ya kuufadhili mradi huo, na sasa wapo kwenye hatua za mwisho za mapitio ili kutoa fedha za utekelezaji, na hiyo ni hatua ya utekezaji wa ahadi yake aliyowaahidi wananchi mwaka jana akiwa kwenye ziara yake mkoani Mtwara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala ndg. Adrew Mgaya amempongeza Mhe. Rais kwa ahadi zake za kweli zinazotekelezeka, huku akieleza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni hatua kubwa ya kuinua uchumi wa Taifa na wananchi wa kawaida, hivyo halmashauri imejipanga kutumia fursa hiyo kuongeza pato kwa kuboresha miundombinu yake ya makusanyo.
Kikao hicho kimefanyika jana Jumatano tarehe 20/05/2020 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya mji newala ambapo awali Tanroads ilipanga kufanya vikao kwenye vijiji vinavyopita mradi huo kuongea na wananchi kuwaeleza mambo mbalimbali ikiwemo fidia, faida na athari za mazingira zinazoweza kujitokeza lakini kutokana na uwepo wa ugonjwa corona wameamua kuongea na wawakilishi wa wananchi ili kupunguza hatari ya maambukizi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa