Baraza la Madiwani la halmashauri ya Mji Newala jana 14 February, 2019 limeidhinisha rasimu ya bajeti ya maendeleo ya mapato na matumizi kwa mwaka 2019-2020 yenye thamani ya shilingi bilioni 19,028,167,045/=
Akizungumza mara baada ya kupitisha rasimu hiyo ya bajeti Mwenyekiti wa halamshauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi amewataka madiwani na wataalamu kuwa tayari na kujielekeza kwenye utekelezaji wa bajeti kwa kuunganisha nguvu na kushikamana wakati wa kutekeleza miradi kama ilivyoekezwa kwenye mapendekezo.
Kwa upande Mkurugenzi wa halmashauri, Ndugu Andrew Mgaya, amesema mapendekezo hayo siyo ya moja moja kutokana na miongozo ya kibajeti, kwani hivi sasa serikali inaangalia zaidi miradi mikakati na kwamba imeachana na miradi midogo midogo hivyo upo uwezekano wa kubadilika kwa kuwekewa ukomo wa bajeti kutokana na miradi iliyopendekezwa.
Aidha Mkurugenzi amewapongeza madiwani kwa michango yao ya kubaini vyanzo vipya vya mapato na kuwaomba kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu mradi mipya ya halmashauri inayoenda kutekelezwa ya upimaji ardhi shirikishi, anuani za makazi pamoja na utoaji wa vibali ya ujenzi.
Aidha jumla ya fedha hizo pendekezwa zinazokadiriwa kukusanywa na kutumika mishahara ni shilingi bilioni 13,092,421,545 sawa na 69%, Matumizi mengine ni shilingi bilioni 1,683,554,000 sawa na 9%, miradi ya maendeleo shilingi bilioni 3,963,371,500 sawa na 21% na shilingi milioni 280,000,000/= sawa na 1% michango ya wananchi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa