Halmashauri ya Mji Newala imeidhinishiwa shilingi Bilioni 21.5 kuwa bajeti yake ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 20223/2024 huku Mkuu wa wilaya ya Newala Alhaj. Mwangi Rajabu Kundya akiitaka halmashauri hiyo kutumia fedha za miradi ya maendeleo kwa kuzingatia malengo ya Taifa.
Alhaj. Kundya ameyasema hayo katika mkutano wa baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo wa robo ya nne 2022/2023 uliofanyika Agosti 03, 2023 na kuhimiza uadilifu katika usimamizi ili kupata matokeo bora yakujivunia kwa kuwa kupata fedha za kutekeleza miradi kutoka serikali kuu ni fursa.
Aidha ameeleza kuwa hali ya utekelezaji wa miradi ni ya wastani hivyo uadilifu na uaminifu uongezeke ili ikamilike kwa wakati na katika ubora, “ndugu zangu kupata miradi ni fursa.. fursa muhimu sana… fursa ambayo huko nyuma ilikua inapatikana kwa bahati nasibu… tuzitumie fursa hizi”. Alilisitiza Kundya.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka waheshimiwa madiwani kuweka kipaumbele katika usimamizi utakaosaidia kubaini mapungufu kwa kuwa hilo ni jukumu lao la kusimamia maendeleo ya halmashauri na sio kuwaachia wataalam peke yao ambao baadhi yao wameonekena kutokuwa waadilifu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Yusuph Kateule amewaangiza madiwani kushirikiana na watendaji wengine wa halmashauri kuhakikisha kila chanzo cha mapato kilichoainishwa kwenye mpango wa bajeti kinakusanywa kikamilifu katika maeneo yao.
Aidha Mhe. Kateule ameonya matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa wataalam na kuwataka kufanya matumizi kwa mujibu wa mpango wa bajeti na vipaumbele vyake vinavyolenga kutoa majibu ya maendeleo kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye ameomba ushirikiano na umoja pamoja na kumtanguliza Mungu toka kwa wasimamizi, madiwani na wataalum kwa kuwa hiyo ndio njia pekee ya kufikia mafanikio katika kuwatumika wananchi.
“Ndugu zangu tukimtanguliza Mungu mbele nina imani kabisa tutavuka salama, na lengo lile la kuwatumikia wananchi wetu tutalitimiza kwa madhumuni hayo amabayo tutakuwa tumeyaweka”. Alieleza Mkurugenzi huyo.
Bi. Sophia Makungu Afisa Miapango wa Halmashauri hiyo katika mkutano huo ameainisha mchanganuo wa bajeti hiyo kuwa, shilingi bilioni 11.9 ni mishahara na matumizi mengine ya ofisi, Ruzuku ya mairadi ya maendeleo kutoka serikali kuu ni shilingi bilioni 3.9.
Shilingi bilioni 2.6 fedha kutoka kwa wahisani, Makusanyo ya mapato ya ndani shilingi bilioni 2.6 pamoja na mchango wa jamii shilingi milioni 280 unaotokana na shughuli za kujitolea nguvu kazi wakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa