Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Newala mkoani Mtwara, kimeridhishwa na mafanikio yaliyopatikana katika jimbo la Newala Mjini yaliyotokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho kuanzia Novemba 2015 hadi Decemba 2018.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani Jumatano January 09,2019 kwenye kikao cha halmashauri kuu ya jimbo la Newala Mjini cha kupokea taarifa hiyo mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amesema toka serikali ya awamu ya 5 ya Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania imeingia madarakani chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mafanikio yaliyopatikana jimboni humo ni makubwa.
Ameyataka baadhi ya mafanikio yaliyopatika kwenye sekta ya afya kuwa ni uboreshaji wa zahanati ya Mkunya kuwa kituo cha afya, kukamilisha zahanati ya Mwanona na kuanza kutoa huduma, ujenzi wa zahanati 8 mpya, zahanati ya Tupenadane, Mcholi Godauni, Moneka, Mkulung’ulu, Chitandi, Mandumba, Amani na Msilili, ambapo zahanati za Mwanona, Chitandi, Mcholi Godauni na Mkulung’ulu zimesajiliwa.
Mafanikio mengine baadhi katika katika hospitali ya wilaya ni kuweka mfumo ya kielektronic ya kukusanya mapato, kuanzisha duka la dawa, machine ya usingizi, mashine 1 ya kutolea dawa ya usingizi, mashine 1 ya kupima damu, gari 1 la kubeba wagonjwa, mashine 2 za kufulia na ukarabati wa chumba cha watoto wa njiti na mashine zake.
Aidha Mkuu wa wilaya amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye sekta ya elimu hasa katika ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, maabara za shule, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, mabweni na hata matokeo ya hivi karibuni darasa la 7 na kidato cha 6 inaonyesha halmashauri ya mji Newala imekuwa kunara.
Hata hivyo hivyo amesema mafanikio hayo yapo katika idara zote na hiyo inatokana na kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa hamashauri chini ya Mkurugenzi wao, Ndugu Andrew Mgaya ambaye amekuwa msimamizi nzuri wa fedha na nidhamu ya utendaji kazi kwa watumishi.
Kwa namna ya pekee amempongeza Mbunge wa jimbo hili ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora Mhe. George Mkuchika, kwa kuwajali wananchi wake kwani amakua mstari wa mbele kufanikisha shughuli za maendeleo kwa kutafuta wahisani na fedha za mfuko wa jimbo kitu ambazo wambunge wengi wanashindwa kufanya hivyo nakuangalia maslahi yao binafsi.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Mhe. George Mkuchika amesema bado ataendelea kuwatumikia wananewala katika mahitaji yao ya maendeleo kwani wao ndio waliompa dhamana hivyo wasitegemee kama atawaangusha kwani japo kazi aliyoifanya inaonekana lakini bado ataendelea kushirikiana nao na kukitumikia Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya chama.
Sambamba na hilo amekishurukuru chama kwa kumpa ushirikiano katika kutekelezaji wa majukumu yake na kuwaomba wanachama ushirikiano zaidi katika kipindi kilichobaki huku akitoa pongezi kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala na watendaji wake kwa kuwa mwaminifu katika usimamaizi wa fedha.
Akipokea taarifa hiyo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani Newala na mwenyekiti wa kikao hicho ndugu Jabir Mtanda, amesema wameridhishwa na matokeo ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi zinazotokana ilani ya CCM kwa kipindi hiki cha miaka 3 na wataendelea kuwasimamia watendaji wa serikali ili kuhakikisha serikali inafikia malengo yake.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa