Hali ya afya na lishe ya watoto ndani ya halmashauri ya Mji Newala imeendelea kuimarika kutokana na jamii kupata uelewa pamoja na kujitokeza kushiriki katika masuala yanayohusu lishe.
Hayo yamebainishwa na afisa lishe wa halmashauri hiyo Bi. Beatrice Saria katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani katika zahanati ya Tupendane iliyopo kata ya Tulindane ambapo amesema inatokana na jamii kujihusisha moja kwa moja katika lishe.
“wazazi wameweza kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho tunayoyafanya kila robo, katika shughuli zetu za kila siku na elimu tunazotoa kupitia mikutano ya kijiji, kwa njia ya redio kwahiyo tunaona kuna mabadiliko makubwa na kuna tofauti ya mwanzo na sasa.”
Aidha ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo wazazi 2550 wamepata elimu ya unyonyeshaji maziwa ya mama, watoto 1750 wamefanyiwa tathmini ya hali ya lishe na 14 kati yao saw ana 0.8% ndio waliokutwa na ukondefu pamoja na wazazi 980 wenye watoto wa miezi 0-23 wamepatiwa unasihi wa ulishaji watoto wadogo na wachanga.
Ndugu Chibwana Fadhili kutoka kitongoji cha Mfalanyaki mzazi aliyemleta mtoto wake kupimwa hali ya lishe na kupata elimu amesema malezi ya mtoto yanawahusu wazazi wote hivyo yeye kama baba anawajibu wa kusimamila jukumu hilo.
Bi. Fadhila Musa mkazi wa Mnuwi amesema maadhimisho yamempa faida kubwa ikiwemo kupata elimu ya unyonyesha huku akiiomba jamii kushirikiana katika malezi ya mtoto kwa kuwa malezi bora yanaleta ukuaji bora.
Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani yalianzia agosti 1-7, 2025 yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo “Thamini Unyonyeshaji: Weka Mazingira Wezeshi Kwa Mama Na Mtoto.”
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa