Halmashauri Nchini zimetakiwa kuendelea kuhifadhi mazingira, kuanzisha sheria ndogo ndogo za utunzaji mazingira pamoja na kutenga bajeti zitakazo wezesha shughuli za utunzaji mazingira.
Agizo hilo limetolewa na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Atupokile Mhalila wakati anatoa salamu za mwenge kwa wananchi wa kijiji cha Amani kilichopo Kata ya Mcholi 1 wakati mbio za mwenge zilipofika kijijini hapo kuzindua nyumba ya mtumishi wa zahanati ya kijiji.
Bi. Mhalila amesema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zimebeba ujumbe mkuu unaohimiza uhifadhi wa mazingira hivyo Halmashauri kama chombo kinachotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii zinazo wajibu wa kuboresha sheria na kuongeza usimamizi.
Aidha amewataka wananchi wa Newala kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti hovyo, kutupa taka bila kuzingatia uhifadhi wa mazingira na kufanya kilimo karibu na vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunapelekea hali ya ongezeko la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwa na, ukame, uhaba wa mvua, mlipuko wa magonjwa pamoja na joto kali.
Katika Halmashauri ya Mji Newala Mwenge wa Uhuru unatarajia kutembelea miradi tisa ya maendeleo na mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi Zahanati ya Amani umetokana na mapato ya ndani ya halmashauri na umetekelezwa kwa Force Account ukiwa na thamani ya shilingi milioni 52.452 kati hizo shilingi laki 5 ni mchango wa nguvu za wa wananchi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhishwa na hatua za ujenzi na kuridhia ufunguzi wa matumizi ya nyumba hiyo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa