Halmashauri ya Mji Newala imeibuka kuwa kinara kwa kufaulisha wanafunzi walifanya mtihani wa matokeo ya darasa la 7 mwaka 2019 mkoani Mtwara, katika matokeo yalitangazwa hivi karibuni tarehe 15/10/2019 na baraza la Mitihani nchini NECTA.
Katika matokeo hayo halmashauri ya mji Newala yenye shule za msingi 45, imeshika nafasi ya 12 kitaifa sawa na ufaulu wa asilimia 94.04 kwa wanafunzi wote 1,896 waliofanya mtihani huo, wavulana 898 na wasichana 998, ambapo kati yao wavulana 852 wamefaulu na wasichana 931.
Ofisa Elimu Msingi wa halamsahauri hiyo Mwl. Mohamed Mwende amesema, mafanikiwa hayo hayakuja kwa bahati mbaya bali ni jitihata na mipango ya pamoja baina ya ofisi yake, waalimu, wazazi, pamoja na wanafunzi wenyewe kuzingatia walichofundishwa darasani.
Hata hivyo amefafanua kuwa, wanajivunia mafanikio hayo kwa kuwa tangu mwaka 2016 ufaulu umekua unapanda kwani 2016 ufaulu ulikua 60% nafasi ya 5 kimkoa na 145 nafasi ya kitaifa, mwaka 2017 ufaulu ulikua 72% nafasi ya 3 kimkoa na 90 nafasi ya kitaifa, mwaka 2018 ufaulu ulikua 91.5% nafasi ya 1 kimkoa na 12 nafasi ya kitaifa sawa na mwaka huu 2019 huku ufaulu ukifikia 94.04%.
Aidha ameeleza kuwa agizo alilolitoa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa mapema mwaka jana 2018 la kuzitaka shule zote mkoani humo kuhakikisha zinamaliza kufundisha mtaala mwezi juni, limesaidia kuwaanda wanafunzi vizuri, kwa kubaini mapungufu mapema na kuyafanyia kazi kabla ya mtihani.
Sambamba na hilo Mwl. Mwende amewataka wazazi kuhakikisha wanawandaa mapema watoto wao na masomo ya sekondari, na hiyo ndiyo fahari pekee na matunda ya kazi waliyoifanya na kwa namna yoyote ile waepuke kuwawekea vikwazo vya kutowaendeleza kimasomo kwa kuwaozesha au kutogharamia mahitaji yao ya shule.
Katika hatua nyingine amewataka wazazi wenye watoto wa umri wa miaka 4-5, kwenda kuwaandikisha kwenye madarasa ya awali kwani baada ya miaka miwili watoto wataoandikishwa darasa la kwanza ni wale waliopo kwenye madarasa hayo tu, kwani wao ndio watakua wameandaliwa kwa ajili ya kupata elimu ya msingi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa