Halmashauri ya Mji Newala kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepokea shilingi bilioni 3.38 kutoka serikali kuu na wadau wamaendeleo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.
Hayo yamebainishwa na mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu Mkuu wa wilaya Newala Mhe. Mwangi Kundya ambapo ameeleza kuwa serikali imelenga kupunguza changamoto na vikwazo katika elimu.
“Fedha hizi zimetekeleza miradi ya Boost, Sequip, EP4R pamoja na miradi ya ufadhili wa BARICK ili kuhakikisha jamii yetu inapata elimu kamilifu, na kuweza kumudu ushindani katika ulimwengu”
Aidha Mhe. Kundya amesema katika kuongeza kasi ya kuinua elimu serikali imeajiri walimu 49 wa halmashauri hiyo walimu 24 wa shule zamsingi na 25 wa shule za sekondari sambamba na kuwapatia vitabu vya mitaala iliyoboreshwa, vifaa vya maabara, Tehama pamoja vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji kwa madarasa ya awali.
Hata hivyo kutokana na tathmini ya matokeo miaka mitatu, kuwa na ulingano wa ufaulu ameagiza Idara ya elimu kuchukua hatua za kutafuta majawabu ya changamoto yatakayowezesha kuongeza ufaulu.
Kwaupande wake Katibu tawala wa wilaya ya Newala Ndg. Thomas Safari amesisitiza suala la nidhani njema na mavazi kwa walimu pamoja na walimu kuonyesha upendo kwa wanafunzi vitasaidia kuongeza kiwango cha taaluma.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye amewaomba watumishi hususani walimu kupunguza fikra za kutaka uhamisho kwa kuwa ni moja ya chanagamoto inayoikabili idara ya elimu na kwa wale wanaotaka kufanya hivyo wafuate utaratibu.
Akizungumzia maadhimisho hayo Mkuu wa idara ya elimu sekondari Mwl. Diana Sonno amesema lengo la juma la elimu ni kuboresha ujifunzaji na ufundishaji kwa kufanya tathmini ya kwa kushirikiana na wadau wa elimu saw ana lengo la serikali.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa