Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Gaspar Byakanwa, leo Ijumaa December 14, 2018 ametoa pongezi kwa halmashauri ya Mji Newala, kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika ufaulu wa wananfunzi wa darasa la saba mwaka huu.
Mkuu wa mkoa ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha pamoja kati yake na wakuu wa wilaya, makatibu tawala, wakurugenzi wa halashauri, wenyeviti wa halmashauri na maafisa elimu wa mkoani hapa, kikao kilichofanyika mjini Newala kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Newala.
Hata hivyo Byakanwa amesema japokuwa mkoa kwa ujumla umejitahidi kutimiza malengo yake ya kitaifa ya kufaulisha wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza 2019, kwa kushika nafasi ya 8, kutoka nafasi ya 26 mwaka jana 2017 bado halmashauri ya Mji Newala ni ya mfano kwani imetekeleza makubaliano.
Aidha Mkuu wa mkoa ameitaka halmashauri ya Mji kutobweteka na matokeo hayo badala yake iongeze juhudi ili kuendelea kutetea nafasi hiyo huku akiutaka mkoa kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha elimu na kufikia lengo ya kufaulisha kwa asilimia 100 pamoja na kuwa kwenye nafasi 3 za juu za ufaulu kitaifa.
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amempongeza Mkurugenzi wa Mji Newala Andrew Mgaya, kwa mikakati yake ya kukabiliana na changamoto kwenye sekta ya elimu hasa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na uhaba wa madawati kwani halamshauri hiyo haina upungufu wa madawati na ipo kwenye hatua za kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa utakaomaliza tatizo hilo kwa asilimia 100.
“sitaki kuona wanafunzi yoyote anasoma chini ya mti katika mkoa wangu haiwezekani, wakurugenzi hakikisheni hilo halijitokezi na mujadiliane na wabunge wenu fedha za mfuko wa jimbo kipaumbele chake kiwe ni kujenga vyumba vya madarasa na madawati na zoezi hilo ifikapo February 2018 liwe milikamilika, na ninawaagizeni wakuu wa wilaya simamieni kikamilifu zoezi hili katika wilaya zenu na lianze mara moja” amesisitiza Byakanwa
Awali akizungumza wakati anamkaribisha mkuu wa mkoa katika kikao hicho Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Bi. Germana Mung’aho amesema halmashauri ya Mji Newala imefaulisha kwa asilimia 91 na kushika nafasi ya kwanza kutoka nafasi ya 3 mwaka jana ambapo ilifaulisha kwa asilimia 72.
Mung’aho amefafanua kuwa jumla wa wanafunzi 20,100 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019 mkoani hapa, na kati yao wasichana ni 10,943 na wavulana 9157 huku akieleza kuwa huo ni wastani wa mafanikio ya asilimia 100 na kuitaka jamii kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa wanajiunga na masoma na kumaliza.
Ufaulu wa darasa la saba kimkoa mwaka 2018 unaongozwa na 1. halmashauri ya Mji Newala, 2.halmashauri ya Mtwara Vijijini, 3.halmashauri ya Mji Masasi, 4.halmashauri ya Mji Nanyamba, 5.halmashauri ya Mtwara Manispaa, 6.halmashauri ya wilaya Newala, 7.halmashauri ya wilaya Tandahima, 8.halmashauri ya wilaya Masasi na iliyoshika mkia ni 9.halmashauri ya wilaya Nanyumbu
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa