Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Newala kupitia Mwenyekiti wake Mhe. Jabir Mtanda kimetoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala pamoja na wataalamu wake kwa kushirikiana vema na Mbunge wa jimbo hilo katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ameyasema hayo wakati anafunga kikao maalum cha kamati ya jimbo cha kuwasilisha utekelezaji wa ilani ya CCM Januari hadi Juni 2022 kilichofanyika jana Jumamosi 16 Julai 2022 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambapo amesema kutokana na taarifa ya mafanikio ya miradi usimamizi umefanywa na Mkurugenzi na watu wake hivyo wanastahili pongezi.
Amesema chama kupitia ilani kiliahidi mambo kadha ya kuwafanyia wananchi na kwa kupitia Mbunge ambaye pia ni Waziri Mhe. George Mkuchika lazima iwe na timu yakushiriana nayo kufanikisha lengo la serikali la kuwapatia wananchi maendeleo kupitia watumishi waliopo serikalini na kwa jimbo hilo kazi inafanyika kwa ushirikiano mkubwa.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Newala Mji Mhe. George Mkuchika(W) amesema anafurahishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yake huku akiwasisitiza kuacha alama ya maendeleo itakayo kumbukwa na wananchi katika utumishi wao umma wakiwa Newala.
Amesema Newala inahitaji kwenda mbele kimaendeleo kwa kasi kubwa kutokana na hapo awali wananchi walichelewa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na changamoto ya uwepo wa vita katika nchi jirani ya msumbiji ambayo wilaya inapakana nayo na moja ya athari zake ilikuwa ni wananchi kukimbia na kujificha.
Hata hivyo amesema kwa sasa Jimbo limefikia hatua kubwa ya mendeleo katika sekta ya afya kwasasa upo ujenzi wa vituo vipya vya afya viwili, sekta ya elimu ujenzi na hatua za uanzishwaji wa shule mbili za kidato cha tano na sita, ujenzi wa shule mpya ya sekondari makondeko, sekta ya miundombinu ujenzi wa barabara za lami, uborejeshaji na ukarabati kwenye sekta ya maji na maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Newala Mhe. Rajabu Kundya amewataka wajumbe wa kamati ya jimbo kujivunia mafanikio yaliyofikiwa na huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kuyasemea kwenye majukwaa mbalimbali ili wananchi waelewe juhudi zinafanya na serikali yao katika kuwafikishia maendeleo.
Aidha Mhe. Kundya amewaomba wajumbe wa kamati kuendelea kumuunga mkono mbunge katika kuendeleza jidihada za kufanikisha ilani na kuwapatia maendeleo wananchi kwa kuwa kazi hiyo haiwezi kufanywa na mtu mmoja na pasipo kufanya hivyo kutatoa mwanya kwa wengine kuudanganya umma kuwa wao ndio wametekeleza.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo Bi. Sophia Lipenye amesema pamoja na pongezi zilizotolewa kwa Halmashauri Chama hakitaacha kufuatalia utekelezaji wa ilani yake kwa kuwa huo ndio mkataba wao na wananchi hivyo wataalamu wasilale wahakikishe wanawajibika ipasavyo katika kufanikisha majukumu yao.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati waliohudhuria kikao hicho wamesema ni jambo zuri kuona kamati jimbo linaendelea kutekeleza miradi yake kwa kushirisha wananchi kamati za kusimamaia miradi kitu ambacho kinapaswa kuendelezwa kenye kila mradi ili kujenga imani kwa wananchi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa