Halmashauri ya Mji Newala imeweka mkakati wa kuwafikia wakulima katika maeneo yao kuwahamasisha na kuwapa elimu ya kulima mazao ya biashara ili kuyafikia malengo yaliyowekwa na mkoa Mtwara.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Geofrey Nnauye katika kilele maadhimisho ya sikukuu ya wakulima katika viwanja vya maonesho ya nanenane kanda ya kusini kwa kueleza kuwa halmashauri ipo katika kutekeleza mkakati wa kuinua uchumi kupitia mazao ya biashara.
“Na mkakati ambao tumeweka ndani ya mkoa ni kuinua uchumi wa wananchi kupitia kilimo hasa mazao ya biashara na sisi wananchi wetu wa halamshauri ya Mji Newala ni wakulima na tumetengeneza mkakati wakupita kwenye vijiji vyetu kuhamasisha wananchi walime mazao ya kibiashara”.
Kwa upande wake afisa kilimo wa halmashauri hiyo Ndg. Calistus Komba amesema katika maonesho ya mwaka 2025 walijikita katika utoaji elimu kupitia vitalu vya mashamba darasa hasa kwa mazao ya ufuta, alizeti, mpunga, karanga na mazo mengine ya chakula.
Komba ameeleza kuwa “Wananchi wamejifunza kwakweli tunaamini mwaka huu tutakuwa na mafanikio makubwa zaidi ya mwaka jana na pia wataenda kufanya shughuli za kilimo kwa tija, kwa maana ya kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na serikali nayo itaongeza pato”.
Katika hatua nyingine amewataka maafisa ugani wanapotemebea maonesho hayo kutembelea maeneo mengine kwenda kujifunza mbinu na teknolojia mpya ili wakatumie katika shughuli zao za kuwahudumia wakulima.
Afisa kilimo anayeratibu maonesho ya nanenane halmashauri ya Mji Newala Bw. Juma Kahamba amefahamisha kuwa elimu waliyoitoa kwa wakulima wakiizingatia inatosha kuwapatia mafanikio makubwa katika shughuli zao.
Hata hivyo mratibu huyo amewaomba wakulima kuunga mkono juhudi za halmashauri katika kulima mazao tofauti tofauti ya biashara kwa kuwa yanafaida za kiuchumi ambazo hazitegemei mapato ya msimu mmoja.
Halmashauri ya Mji ya Newala pamoja na kutoa elimu ya kilimo bora katika maonesho hayo lakini pia imetoa elimu ya ufugaji, uchaguzi, usaidizi wa kisheria pamoja na kuonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali wa halmashauri hiyo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa