Halmashauri ya Mji Newala imetoa pongezi kwa shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na cha sita mwaka 2019, kwa kuzikabidhi vyeti vya ubora na fedha tasilimu kama motisha.
Hafla ya kukabidhi zawadi hizo ilifanyika mwishoni mwa juma Ijumaa Machi 20, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo na mgeni rasmi aliyekabidhi zawadi hizo ni Mkuu wa wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo ambae ameipongez halmashauri hiyo kwa hatua ya kuthamini mchango wa waalimu.
Mkuu wa Wilaya amesema ni heshima ya pekee kwa waalimu kutiwa moyo kutokana na kazi yao ngumu wanayoifanya kwani wamekua mstari wa mbele kuhakikisha kunakua na ustawi nzuri wa watoto, kuanzia darasani na malezi mengine ya kijamii kama kuwalinda, kuwafundisha heshima na maadili mema.
Aidha Mhe. Mangosongo ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa halmashauri kwa kuwa mkurugenzi bora katika kusimamia maendeleo sambamba na waalimu hao ambao wameamiwa katika kusimamia miradi na shughuli mbalimbali za kitaifa kwa mafanikio.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi ambae ni Afisa Elimu Sekondari Mwl. Athuman Salum amesema halmashauri imeziona jitihada kubwa zinazofanywa na waalimu, hivyo hatua hiyo imelenga kutambua mchango wao ambao una thamani kubwa ili kuongeza hari ya ufundishaji na ufaulu kwa wanafunzi ambao ndio taifa la baadae linalotegemewa.
Akitoa taarifa ya hali ya ufaulu ya halmshauri hiyo Afisa Elimu Msingi Taaluma , Said Kaminya amesema ufaulu kwa halmashauri hiyo umeongezeka toka 91% hadi 94% kwa shule za msingi ambapo kimkoa imekua, kidato cha nne ufaulu umekua 79.81% kimkoa imekua ya tano na kidato cha sita ufaulu umekua 100% na kushika nafasi ya kwanza kimkoa.
Shule za msingi zenye darasa la wanafuzi chini ya 40 zilizopewa zawadi ya fedha na vyeti ya kwanza ni Kikuyu Tsh. 300,000/=, Chikwaya Tsh. 200,00/= ya pili na ya tatu Nanyonda Tsh. 150,000/=, shule zenye wanafunzi zaidi ya 40 ni Likuna Tsh. 300,000/= nafasi ya kwanza, Newala Tsh. 200,000/= ya pili na Mkunya Tsh. 150,000/=
Sekondari Kidato cha nne ya kwanza ni Kiuta Tsh. 300,00/=, Kusini Tsh. 200,000/= na Malegesi Tsh. 150,000/= pamoja na sekondari kidato cha sita ni Kiuta iyopata Tsh. 300,000/=.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa