Halmashauri ya Mji Newala imeishukuru taasisi binafsi ya kitaifa inayodhibiti saratani ya matiti JHPIEGO kwa kuwawezesha matabibu na wauguzi kupata ujuzi wa kufanya uchunguzi na kubaini wagonjwa.
Taasisi ya JHPIEGO chini ya ufadhili wa Pfizer Foundation kwa kushirikiana na wizara ya afya na TAMISEMI hivi karibuni wameendesha kampeni ya siku tano ya uchunguzi wa saratani ya matiti ndani ya halmashauri ya Mji Newala.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Maryrose Giattes amesema lengo lao kuu ni kudhibiti ongezeko la wahanga wa saratani ya matiti kwa kuhakikisha 60% ya wagonjwa wanagundulika katika hatua ya wali sambamba na kuwajengea uwezo wataalam.
Dkt. Giattes ameongeza “vilevile tunawajengea uwezo watoa huduma wa afya wa nne madakatari na manesi pamoja na mtaalam mmoja wa ultrasosund katika kila halmashauri kwenye vituo huduma, waweze kuchukua sampuli na kuzifanyia uchunguzi wa kubaini tatizo”.
Mmjo wa wanufaika wa mafunzo hayo ambaye mtakwimu wa saratani ya matiti halmashauri ya Mji Newala Bi. Hadija Shikila ameshukuru kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa kwasasa wameongeza ujuzi wa kuwabaini wagonjwa wenye dalili ya saratani ya matiti.
Aidha Bi. Shikila ambaye pia ni muuguzi msaidizi katika hospitali ya wilaya ya Newala ameeleza kuwa kwasasa wapo tayari kutoa huduma ya uchunguzi hospitalini hapo hivyo wananchi wajitokeze kupata huduma.
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Rashid Suleiman ameeleza mafunzo hayo yamehusisha namna ya kufanya uchunguzi kupitia njia ya kupapasa titi na uchunguzi wa ultrasound kwa kuchukua vinyama kwenye matiti au maji maji.
“mafunzo haya tunatoa darasani kuelekeza, kwa kutumia midoli na vifaa vifaa vingine lakini pia tunawaekeleza kwa njia ya vitendo namna ya kupapasa titi, kuchukua vinyama na maji kupitia kuchoma sindano na uchunguzi wa ultrasound.” Ameeleza Dkt. Suleimani
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa