Hotuba ya Mhe. Rais Magufuli Wakati wa Kuwaapisha mawaziri wapya leo tarehe 12/11/2018 Ikulu Dar es salaam
RAIS MAGUFULI: Kwa namna ya pekee niwapongeze waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Kilimo na Viwanda kwa kufika kwenu. Kuna gazeti linanikumbusha kuwa Mawaziri 20 nilioanza nao wamebaki 11 na 9 nimewatengua. Nimejiuliza miaka 2 iliyobaki wangapi watakuwepo?
RAIS MAGUFULI: Katika kazi hizi za kuleta maendeleo na kufikia malengo sio lazima wote mfike. Kuna mambo ambayo tulijiwekea malengo ya kuyafikia ikiwemo sekta ya Kilimo na Viwanda. Wizara hizi zinauwezo wa kutatua changamoto ya ajira
RAIS MAGUFULI: Sekta ya Kilimo na Viwanda ni sekta nyeti na mara nyingi nimekuwa nikigombana na Waziri Mkuu nikimuuliza mbona hiki hakiendi? Mara nyingine nampigia simu saa 8 usiku nikimtuma huku na huku kwasababu ndio kiranja wa Mawaziri
RAIS MAGUFULI: Nimekuwa nikiona Wizara zinazofanya kazi vizuri. Ukienda TAMISEMI kuna vijana wanafanya vizuri, Seleman Jaffo. Nimetoa mfano wa huyu kwasababu ndio kijana mdogo na nimesikia ana wake wanne
RAIS MAGUFULI: Limetokea suala la Kahawa nilimtuma Waziri Mkuu akaenda kulishughulikia. Tena wengine wanaovuka mpaka kwenda kuuza Kahawa wanatokea kwa Waziri Mwijage nikajiuliza au ameegemea kwenye Viwanda amesahau Biashara?
RAIS MAGUFULI: Kuna kiwanda kilikuwa kimekaa bila ya uzalishaji nikamtuma Waziri Mkuu akaenda kutatua Mpaka nikamwambia sasa nitakufanya uwe Waziri wa Viwanda au Kilimo
RAIS MAGUFULI: Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha Korosho kwa wingi Duniani. Tumebahatika kupata Bunge kama chombo cha kutunga sheria, taasisi na Bodi mbalimbali lakini linapokuja suala la mazao ya Watanzania siwaoni wakifanya juhudi
RAIS MAGUFULI: Mkurugenzi wa TANTRADE hajui kama anatakiwa kutafuta masoko ya mazao yetu au yeye anasubiri tarehe 1 mwezi wa 7 ili afungue maonesho ya saba saba. Mkurugenzi wa TANTRADE anasubiri kupokea viingilio vya maonesho ya saba saba
RAIS MAGUFULI: Kulikuwa na kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu na Mimi nikaona nivamie na Waziri Mkuu hakunifukuza nikafurahi. Niliyoyasikia humo yaliniumiza, Mwakilishi wa Bodi ya Korosho nilimuuliza bei ya Korosho akasema Tsh. 1,000 na Bei elekezi waliyoitoa ni 1,500
RAIS MAGUFULI: Niliangalia mataifa mengine nikaona bei ya Korosho imeshuka kidogo India. Nikaona Bodi ya Korosho haipo kwaajili ya manufaa ya Watanzania. Nikawapa bei elekezi ya Tsh. 3000 lakini siku ya mnada waliongeza shilingi 1 aliyeongeza zaidi alinunua kwa 3016
RAIS MAGUFULI: Nikagundua huu ni mchezo uliopangwa ili mvua ikianza wakainunue Korosho kwa bei ya chini kwasababu Wakulima wataogopa kuharibikiwa. Lakini kwenye hili sikuona statement ya Waziri wa Kilimo wala Viwanda
RAIS MAGUFULI: Nimeamua yafuatayo. Walioleta mapendekezo kwako achana nao watakuja kuleta masharti. Wanaoendelea kuja wala wasihangaike nimeshafunga. Korosho tunanunua wenyewe.
RAIS MAGUFULI: Nimepiga mahesabu ingawa Mimi si mchumi, ukibangua Korosho Kg 3 unapata Kg 1 ukichukua Tani laki 2 utapata Kg elfu 73 na ukigawa kwa Watanzania kila Mtu anapata Kg 2 na Korosho zitakuwa zimeisha
RAIS MAGUFULI: Ile Korosho tutainunua kwa Tsh. 3300 na kila Mkulima alipwe bila ya kukatwa hela yoyote. Maghala yote yalindwe na JWTZ na wameshakaa tayari kusimamia zoezi hili ili Korosho mbaya kutoka nchi jirani huwa inaletwa
RAIS MAGUFULI: Korosho nyingine itapelekwa kwenye Kiwanda kilichopo Lindi kilichorudishwa kwa Serikali juzi kinauwezo wa kubangua tani 73 elfu. Na kuanzia leo Kiwanda hiki nimelipa Jeshi na wao wakishindwa kikiendesha nitawapa wengine. Jeshi liende likakizingire
RAIS MAGUFULI: Korosho yetu ni daraja la kwanza duniani lakini Wananchi wanaishi maisha ya chini na mabodi yapo tu. Tunabaki kuwasikiliza matapeli wanaozungumza kwenye vyombo mbalimbali kwa faida zao na wanaowatuma
RAIS MAGUFULI: Niliowateuwa mkaanze kufanya kazi leo. Tatizo hamfanyi kazi kwa kushirikiana nendeni mkaanzishe ushirikiano. Benki ya Wakulima watatoa fedha na Jeshi litaichukua Korosho na hakuna itakayoibiwa Mimi nawajua. Jeshi likabangue kwa namna watayoona inafaa
RAIS MAGUFULI: Taasisi ya Uwekezaji ihamie kwa Waziri Mkuu na itakapokuwa chini ya Waziri Mkuu hata Mimi nitakuwa na uwezo wa kusimamia. Kuna wawekezaji wa ajabu wamekuja nchi hii. Mtu anakwambia anawekeza Bagamoyo lakini anakwambia usiwekeza hadi Pangani
RAIS MAGUFULI: Tusifikirie wawekezaji wanakuja kutusaidia. Kuna mambo ya ajabu kabisa tena mkataba unawapa kwa miaka 99. Tumekuwa na Bodi zisizofanya kazi.
RAIS MAGUFULI: Sitajali kubadilisha Mawaziri kila wakati hata kama watakuwa wanabadilishana kila baada ya miezi 5. Zao la Korosho limeingiliwa sana hata Wanasiasa walikuwa wanaweka watu wao na kufanya biashara ya 'Kagomba'. Na ndio wasemaji wakubwa wa watu wa huko
RAIS MAGUFULI: Nawapenda wote lakini kwenye ukweli lazima tuambiane. Benki Kuu mwende mkalisimamie hili kuna watu wanataka kuleta fedha za utakatishaji kwenye benki zetu. Wengine walitaka kuingiza Bilioni 150 kupitia benki flani kwahiyo Gavana endelea kubana hivyo hivyo
RAIS MAGUFULI: Unisamehe Jaffo nimekusifu hadharani na Utumishi nimeona nimuongezee Mzee wetu Mkuchika kwasababu alibaki peke yake hata Mtu wa kumtuma alikuwa anakosa. Jaji Mkuu nitakuletea majina ya Majaji wanaochukua rushwa
RAIS MAGUFULI: Jaji Msofe tumekuteua kwasababu umestaafu kwa rekodi nzuri. Pia Jaji Mkuu ninakushukuru kwa ushauri wako na nitakuletea majina ya wanaofanya vibaya. Mawaziri mlioteuliwa msidhani mtapendwa na baadhi ya Wabunge
RAIS MAGUFULI: Baada ya kutangaza mabadiliko Dkt. Tizeba alinipigia simu, nikajiuliza nipokee au nisipokee maana nisije nikaonge kitu watu wakazimia. Lakini alikuwa akinishukuru kwa kuhudumu kipindi chote bila ya kuishia jela
RAIS MAGUFULI: JWTZ nendeni mkafanye kazi hakuna mlilowahi kushindwa. Ukuta wa Mirelani mlijenga miezi 3 badala ya 6. Hii oparesheni ya Korosho haiwezi kuwashinda. Pangeni vikosi vya kubangua Korosho, tukikosa wanunuzi tutazila maana ni kilo 2 tu kwa kila Mtanzania
RAIS MAGUFULI: Wakulima wa Zabibu wanalalamika na Wizara ya Fedha, Viwanda na Kilimo zipo kwanini wanashindwa kutatua. Sio kila kitu mpaka Mimi niseme. Sasa hili la Zabibu mwende mkalimalize sio mpaka niseme mkalimalize
RAIS MAGUFULI: Hao wanaosema tunatumbua ni wachonganishi. Waziri Mkuu nenda ukasimamie hili bei ya Korosho ni Tsh. 3300 hata tukipata hasara potelea mbali. Kokoa kule Kyela mkaifuatilie kwasababu Wananchi wananiandikia 'vimeseji'
RAIS MAGUFULI: Makatibu Wakuu wa Wizara nilizozifanyia mabadiliko msifikirie nimewasahau au kwamba ninyi ndio mmetulia sana. Kuna mambo yanakwama kwasababu ya Makatibu Wakuu. Mwende Mkabadilike
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa