Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Mwariko leo Jumatatu Julai 18, 2022 ameiagiza idara ya afya kupitia kitengo cha lishe kuwaongezea ujuzi Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (WAJA) ili watoe msaada wa kuimarisha afya za watu katika maeneo yao.
Ametoa agizo hilo katika kikao cha kamati ya lishe robo nne 2021/2022 kufuatia taarifa ya baadhi ya wajazito kutotumia dawa za kuongeza wekundu wa damu (FEFO) kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo maudhi baada ya kunywa pamoja na imani potofu katika ndani ya jamii.
Amesema jamii kutojua umuhimu wa FEFO unatokana na mambo mengi ikiwa pamoja na kukosa elimu sahihi, maisha duni, ugonvi wa kifamilia, msongo wa mawazo na mambo mengine kama hayo hivyo waja WAJA wakiwezesha wanao uwezo wakuwafikia kirahisi na kuwabadilisha mtazamo
Mkurugenzi amesema “unakwenda kwenye nyumba hakuna cha mwanaume pale hakuna cha nini, yeye mwenyewe yuko very stressed alafu wewe unazungumzia mambo ya kunywa FEFO, yeye anafikiria nikitoka kliniki nitaambiwa mama jiandae unakaribia kujifungua beba sijui hiki, beba hiki, hana hata kanga atafikiria FEFO huyo? yaani kwa hiyo tuangalie reality ya mazingira yetu watu wetu wengi wapo katika hatua gani.
Hata hivyo Bi. Mwariko amefafanua kuwa suala la lishe ni muhimu kuanzia ngazi familia na ndilo linalotafsiri hali halisi ya maisha ya baadae ya mtoto na mwelekeo wa Taifa kwa kuwa kama hakuna lishe bora hakuna kujifunza na hiyo upelekea kukosa fikra pana za maendeleo kutokana na udumavu wa akili.
Akichangia jambo hilo mjumbe wa kamati ambaye pia ni Afisa Afya Mazingira Bi. Beatrice Mahiri amesema vidonge vya FEFO ni kwa ajili ya kuongeza damu na kumlinda mtoto dhidi ya mgongo wazi hivyo ni vema kama elimu ya kutumia vyakula vinavyoongeza damu kama mbogamboga na matunda inaweza kusaidia usalama wa mama na mtoto.
Akitoa taarifa ya lishe ya robo ya nne Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Bw. Enos Kuzenza ametaarifu wajawazito 1942 waliohudhuria kliniki walipatiwa dawa hizo, watoto 19 walipatiwa matibabu ya utapiamlo mkali, kufanya maadhimisho ya siku ya afya na lishe kwenye kata zote 16, wazazi 1856 wenye watoto wa miezi 0-23 walipatiwa elimu ya ulishaji na WAJA pamoja na wazazi 6001 walipatiwa elimu hivyo katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa