Wataalumu wa idara ya afya ya Halmashauri ya Mji Newala wametakiwa kuongeza usimamizi wa mpango wa Taifa wa udhibiti Malaria pamoja na kusimamaia usafi wa mazingira kwa kuwa ugonjwa huo bado unaendelea kuathiri wananchi wengi.
Agizo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Mwangi Rajabu Kundya wakati anaongea na wajumbe wa kikao cha tathmini ya utekelezaji afua za lishe ngazi ya kata, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Newala.
Mhe. Kundya amesema mpango wa kudhibiti malaria upo lakini haufanyiwi kazi kwani takwimu zinaonesha kwa mwezi Januari hadi Disemba 2023 wagonjwa 47,200 sawa na 28.7% kati ya wagonjwa 164,462 waliofika hospitali walikutwa na vijidudu vya Malaria na hali hiyo sio nzuri.
Ameongeza kuwa ugonjwa huo ni hatari na unazuilika lakini jitihada zinahitajika “jitihada za kuzuia malaria zipo lakini hazisemwi na watu, kuonyesha kwamba wanajali wanajikinga na hili, jitihada za kujikinga na malaria ni ndogo sana, na sasa maji kwa maana ya madimbwi, maeneo mengine mazalia ya mbu hakuna nayeshughulika nayo”. Alieleza Mkuu wa wilaya.
Akizungumzia mara baada ya kikao hicho Mkuu wa Kitengo cha Taka ngumu na usafi wa mazingira Bi. Farida Churi amesema Halmashauri ya Mji Newala imeshaweka mkakati wa kukabiliana na chanagamoto utunzaji mazingira kwa kufanya hamasa na ukaguzi kwenye makazi kuhakikisha watu wanafukia vidimbwi vya maji, kufunika visima na mashimo pamoja na kufyeka nyasi ndefu.
Aidha Churi amefafanua kuwa suala la usafi ni jukumu la kila siku la watu wote hivyo jamii inapaswa kuzingatia ili kuepuka maradhi mbalimbali ikiwemo malaria na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu wa mazingira “tushirikiane kwa pamoja katika kuuweka mji safi na kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuzuia ugonjwa wa malaria.” Ameongeza Churi.
Hata hivyo katika hatua ya kukabiliana na changamoto hiyo amewata viongozi mbalimbali hasa katika ngazi ya vijiji na kata kuwa kitu kimoja ili kufanikisha lengo la Halmashauri la kuhakikisha inaondokana na changamoto ya uchafu wa mazingira.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa