Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Mji Newala Mkoani Mtwara, leo Novembe 29, 2018 imeanza kutoa mafunzo ya awali kwa vikundi 27 vya maendeleo, vinavyotarajia kupata mkopo wa shilingi 80,500,000/= kwa wanawake, vijana na walemavu.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za TARURA Newala Mjini, Afisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri hiyo Bi. Frola Barakana amesema mafunzo hayo yanasaidia kuvijengea uwezo vikundi ili viweze kufikia malengo yake nakutekeleza kikamilifu matakwa ya sheria ya mikopo pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Newala Bi Frola Barakana.
Aidha Barakana amefafanua kuwa, kabla ya kutoa mikopo ni vema vikundi vikapata muongozo wa namna ya kutunza kumbukumbu kutokana na mabadiliko na mitazamo mipya inayokwenda sambamba na mahitaji ya shughuli za maendeleo kwa wakati husika.
Mwakilishi wa kundi la vijana Bwana Issa Malimusi na Bi. Kulusumu Mnayahika mwakilishi wa kundi la wanawake kwa pamoja wamesema, mikopo hiyo imewanufaisha kwa kiasi kikubwa kwani imekua mkombozi katika mipango yao ya maendeleo ya kujikwamua kiuchumi, huku wakiipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapatia mikopo.
“mikopo hii ina faida kubwa kwetu kam kwenye kikundi chetu tunafanya shughuli za ufugaji na ubanguaji korosho hivyo niwaobe vijana waendelee kuwa kwenye vikundi na kutembelea maendeleo ya jamii kwa ajili ya kupata ushauri.” alisema Issa Malimusi.
Washiriki wamafunzo kifuatilia kwa makini maelekezo yanayotolewa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TARURA Newala mjini.
Kwa upande wake mwakilishi wa kundi la walemavu Bwana Shaibu Nanyalika, ametoa pongezi kwa halmashauri ya Mji Newala kupitia idara ya maendeleo ya jamii na serikali kwa ujumla, kwa kuliona na kulitambua kundi hilo linalosahaulika na kuwataka maafisa maendeleo waendelee kuwapa muongozo katika hatua za kutekeleza miradi yao, huku akiziomba taasisi zingine kuiga mfano huo.
PICHA ZAIDI
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa