Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Abbas Ahmad Abbas ameitaka jamii, wadau, mashirika na wasimamizi wa sheria wajikite katika kuweka mipango ya kuzuia ndoa za utotoni na matukio ya vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake kwa lengo la kuiweka jamii salama.
Kanali Abbas ameyasema hayo Machi 08, 2023 kwenye viwanja vya shule ya msingi Amani wilayani Tandahimba katika kilele cha maadhimisho siku ya mwanamke duniani kimkoa ambapo ameeleza kuwa serikali na mkoa unachukua hatua za kukabiliana na vitendo vya ukatili lakini wadau mbalimbali wanahitaji kupaza sauti zao kutokanana na changamoto iliyopo.
Mkuu wa mkoa huyo amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau na mashirika mbalimbali katika kutekeleza sheria na makubaliano ya kikanda na kimataifa ya kupinga vita vya ukatili wa kijinsia wa mtoto na mwanamke lakini mkoa unakabiliwa na tatizo la mimba za utotoni na waasirika zaidi ni mabinti walio chini ya miaka 19.
Aidha Kanali Abbas amewata wananchi mkoani Mtwara kuwa na dhamira ya dhati ya kumaliza vitendo vya ukatili kwa familia kuacha kukaa kimya yanapojitokeza matendo hayo pamoja na kuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano wa ushaidi wa matukio yanayojitokeza.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoani Mtwara Mhe. Agnes Hokororo amewataka wanawake mkoani humo kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ndiye mdau namba moja wa usawa wa kijinsia na ndio maana katika serikali yake wanawake amewapa nafasi katika kila idara.
Aidha amewasisitiza wanawake kujikita katika kuinua elimu kwa kuwa mkoa mkoa umekua na muamko mdogo katika elimu na wanaoweza kufanikisha hilo ni wanawake ambao wanashiriki moja kwa moja kwenye mipango ya kuinua elimu.
Nae Jaji wa Mahakama Kuuu kanda ya Kusini Mhe. Rose Ibrahimu amewataka Wanawake wajikite katika kusimamia uchumi wa familia na Taifa kwa kutumia teknolojia sambamba na kutumia teknolojia hiyo katika kutambua haki zao za msingi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake mkoani Mtwara( TPF-NET) kutoka dawati la jinsia Mkaguzi Msaidizi Bahari Sendela amesema mtandao ulianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuondoa na kuzuia ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawanke na wanaume hivyo jamii inapaswa kulitumia dawati hili ipasavyo.
Hata hivyo Sendela ameeleza kuwa vitendo vya ukatili inaendelea kumeshamiri kutokana na ushirikianao hafifu uliopo kati ya Wananchi na vyombo vya dola na kupelekea wananchi kutokua ana imani hasa na jeshi la polisi lakini jeshi peke yake aliwezi bali kwa kuunganisha nguvu ya pamoja itawezekana.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa