Katika kuadhimisha ya siku ya vijana duniani Agosti 12, 2025 jamii imetakiwa kuwapatia fursa na kuwaamini vijana kama njia muhimu ya kuyafikia malengo mbalimbali ya kitaifa.
Rai hiyo imetolewa na afisa vijana wa halmashauri ya Mji Newala Ndg. Victor Mwaike wakati anazungumzia maadhimisho hayo na kueleza kuwa nguvu ya taifa lolote ipo kwa vijana na huu ni wakati wa kuaminiwa katika kutekeleza mambo mabalimbali.
“Tukumbuke ya kwamba 51% ya nguvu kazi ya nchi yetu inategemea vijana hivyo uwezeshaji wa vijana ni jambo lamsingi na jambo la muhimu sana kwa ajili ya maendeleo endelevu ya taifa letu”
Hata hivyo Mwaike amewata vijana kujikita katika kuzingazia fursa mbalimbali zikiwemo za kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kupata mikopo inayotolewa na serikali kupitia halamashauri badala ya kusubiri na kukata tamaa.
“Kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka 2025 isemayo Uwezeshaji Wa Vijana, Kwa Kesho Endelevu, Vijana wanakila sababu ya kuweka mazingira wakuwezeshwa kiuchumi, ipo mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri na ipo mifuko ya vijana.”
Aidha Halmashauri ya Mji Newala imeadhimisha siku hiyo katika kijiji cha Mcholi Godauni kata ya Mtumachi kwa kutoe elimu na hamasa katika nyanja ya uwezeshaji vijana kiuchumi, elimu, siasa pamoja na kufanya bonanza la michezo kwa vijana.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa