Mkuu wa Jeshi la magereza wilayani Newala SSP Sauli Mayage, amewaongoza maafisa wa jeshi hilo kuchangia damu pamoja na kufanya usafi katika hospitali ya wilaya ya Newala ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho ya kutimiza miaka 64 ya jeshi hilo baada ya uhuru
Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Scolastica Lugenge kwa niaba ya Mganga mkuu wa halmashauri ya Mji Newala amelishukuru jeshi hilo hasa kwa kitendo cha uchangiaji damu kwa kuwa kimesaidia kuokoa maisha ya watu kuongeza akiba ya damu.
“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa jeshi la magereza kwa kujumika nasi wanapozindua sherehe zao za kutimiza miaka 64 baada ya uhuru, shughuli ya kuchangia damu imesidia kuongeza store za damu na pia kuokoa maisha.” Ameeleza Daktari huyo
Aidha Dkt. Lugenge ameziomba taasisi zingine za umma na kijamii pamoja na jamii yote kwa ujumla kuiga mfano huo wa kujitokeza kuwafariji wagonjwa na kuhamasishana katika ushiriki wa uchagiaji damu.
Kwa upande wake afisa afya wa halamshauri ya Mji Newala Bi. Beatrice Mahiri ameeleza kuwa masuala ya afya na usafi wa mazingira ni ya muhimu kwa ajili ya kuepuka maradhi mbalimbali yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.
“Nawashukuru sana kwa maamuzi amabyo walichukua kuja kutusaidia udafika katika hospitali yetu na kwa kweli wamefanya usafi vizuri wamesawazisha baadhi ya maeneo ambayo yalikua hayaja kaa vizuri kuzunguka jengo la dharula, wamedeki jengo na njia zake”.
Hata hivyo ameitaka jamii kuwa na tabia ya kuweka mazingira yao safi kwa kushiriki siku za usafi na kamapeni zinazoandaliwa katika maeneo ya taasisi za umma, ofisi za umma, hospitali, shule na mengineyo kwa ajili ya kujilinda na uchafu.
Jeshi la Magereza nchini limezindua maadhimisho ya kutimiza miaka 64 baada ya Uhuru tarehe 23/08/2025 na kilele chake kitakuwa tarehe 26/08/2025 chini ya kaulimbiu isemayo “Ushirikiano wa Jeshi La Magereza na Jamii, Kwa Urekebishaji Wenye Tija”.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa