Wasimamizi wa miradi ya maendeleo wameshauriwa simamia miongozo inayotolewa pamoja na kushirikisha wadau husika kabla na wakati wa utekelezaji ili kuleta uelewa wa pamoja.
Ushauri huo umetolewa Agosti 07, 2025 na Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye, katika ya ziara ya kamati hiyo yar obo ya nne 2024/2025 ya kukagua ya miradi ya maendeleo.
“Kama katikati wakati wa utekelezaji kuna changamoto tumepitia na kuna mamlaka zingine zimetembelea na kutoa mapendekezo, ushauri tunatakiwa kurudi kwa watu wapewe taarifa, ili kujenga uelewa kwa wote” Nnauye amewashauri wasimamizi wa miradi.
Aidha Mweyekiti Nnauye amewasisitiza wahandisi, kuwasimamia kikamilifu mafundi katika hatua zote na kuwapa ushuri wa kitaalamu, utakao ondoa maswali na kufanikisha ukamilishaji wa miradi katika ubora unaofaa.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walishauri wakati wa utekezaji wa miradi hiyo unaendelea huduma zingine zizingatiwe hasa huduma ya maji ili kuleta ufanisi wa matumizi baada ya kukamilika kwake.
Kamati hiyo ilitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la kituo cha walimu eneo la tupendane, mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu 2 kwa 1 shule ya msingi Nambunga pamoja na ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nambunga.
Kamati hiyo kwasasa inaundwa na wajumbe wa kamati ya wataalam wa halamshauri baada ya kukasimishwa madaraka hayo kwa mujibu wa sheria kutokana na kuvunjwa kwa mabaraza ya madiwani mara baada ya kufikia ukomo wake.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa