Kamati ya Lishe ya halmashauri ya mji Newala, imewataka wafanyabiashara wanaouza chunvi kuacha kusambaza chunvi isiyo na madini joto na kuwasisitiza kuwa kufanya hivyo ni kudumaza afya za watumiaji na ni uvujifu wa sheria.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Lishe wa halamashauri hiyo ambaye pia ni katibu wa kamati hiyo Bw. Enos Kuzenza, wakati anawasilisha taarifa ya utekelezaji ya robo ya kwanza July- Septemba 2019/2020 katika kikao cha kamati hiyo, kilichofanyika Jumatano tarehe 23/10/2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa halamshauri.
Kuzenza amesema japokuwa elimu inatolewa mara kwa mara lakini bado wafanyabiashara wamekuwa wakikiuka utaratibu na katika kipindi cha July-Septemba wamewakamata na kuteketeza chunvi isiyo na madini joto kilo 250 pamoja na kuwatoza faini baadhi ya wafanyabiashara kutokana na kuuza chunvi hiyo kwa wananchi.
Hata hivyo kwa pamoja wajumbe wa kamati hiyo, wameitaka idara ya Afya kuhakikisha inasimamia udhibiti wa uingizwaji chunvi isiyo na madini joto kwa kushirikiana na wataalamu ngazi ya mkoa kufanya vipimo vya kiwango cha madini joto kule inakozalishwa kwenye mashamba kabla hawajauziwa wasambazaji na wauzaji wengine.
Kwa upande mwingine Mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt. Joseph Fwoma, amesema zipo faida nyingi kwa mabinti wenye umri wa kupata mtoto na wamama wajazito kutumia dawa za kuongeza wekundu wa damu (FEFO) sambamba na watoto wa umri chini ya miaka mitano kupata matone ya vitamini A.
Dkt. Fwoma amefafanua kuwa, dawa hizo pamoja na matone ni kinga kwa mtoto kuanzia anapokuwa tumboni na baada ya kuzaliwa, kwa kuwa anakingwa na magonjwa kama mgongo wazi na uono hafifu, hivyo wazazi hasa wajawazito wanapaswa kujitokeza kwenye vituo vya afya ili wapate kinga na tiba kwa ajili ya usalama wao na mtoto katika hatua za uzazi na malezi.
Katika taarifa hiyo ya utekelezaji ya robo ya kwanza 2019/2020, imeeleza kuwa elimu ya vitamin A imetolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa 139%, kuongeza upatikanaji wa nyongeza ya vitamin A, kuongeza ununuzi wa FEFO, asilimia 80 ya wajawazito wamepatiwa FEFO pamoja na sampuli 20 zilipelekwa maabara ya mkoa kwa ajili uchunguzi na sampuli 18 zimegundulika kutokuwa na madini joto kwa 0%.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa