Kamati ya Mfuko wa Jimbo ya hamashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara, jana Novemba 26, 2018 imefanya kikao cha kupokea na kuchambua maombi ya miradi ya jamiipamoja ana kuidhinisha Shilingi 33,600,000/= itakayotumika kwenye miradi hiyo.
Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa wialaya chini ya mwenyekiti wake Mbunge wa jimbo la Newala mjini ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala bora Mhe. George Mkuchika, ambapo kikao hicho kiliamua kupeleka fedha hizo kwenye miradi inayogusa wananchi moja kwa moka kama ilivyo kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati inapenda kuutarifu umma kuwa Mgawanyo wa matumizi ya fedha hizo umegusa Tarafa zote mbili za halmashauri hiyo na mairadi iliyoidhinishwa ni miradi ya ujenzi na ununuzi wa baiskeli za walemavu, ambapo kwenye mradi wa ujenzi Tarafa ya Mkunya imeidhinishiwa fedha Tsh. 14,000,000/=.
Kati ya fedha hizo Tsh. 4,000,000/= zimeelekezwa kwenye umaliziaji wa nyumba ya waalimu shule ya sekondari Malocho, Tsh. 1,200,000/= kukamilisha matundu ya sita (6) ya vyoo shule ya msingi Kiuta, Tsh. 2,000,000/= ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Mpilipili, Tsh. 3,000,000/= ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Amani, na Tsh. 3,800,000/= zimeidhinishwa kwenda kutekeleza ujenzi wa nyumba ya waalimu shule ya msingi Matokeo.
Tarafa ya Newala imeidhinishiwa Tsh. 13,600,000/= kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya ujenzi, ambapo Tsh. 2,000,000/= zitatumika kujenga kisima shule ya sekondari George Mkuchika, Tsh. 4,100,000/= kwa ajili ya kujenga darasa katika shule ya msingi Kilidu, Tsh. 2,000,000/= kwa ajili ya kumalizia ofisi ya kijiji cha Mahumbika, Tsh. 2,000,000/= kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Moneka, Tsh. 1,500,000/= ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Makote, na Tsh. 2,000,000/= kwa ajili ya kumalizia Ofisi ya Mtaa Majengo.
Kamati pia imeidhinisha Tsh. 6,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli 10 za walemavu ambao wanne kati yao ni wanafunzi na kamati imeamua kuwapa kipaumbele ili kuendana na sera ya Taifa ya elimu sawa kwa wote sambamba na sera ya elimu bure.
Wanafunzi hao wanaotarajia kupata baiskeli hizo ni Sharibu Hassan wa shule ya msingi Julia, Samko Muksini wa shule ya msingi Tupendane, Zuhura Mohamedi wa shule ya msingi mkoma 1 na Savia Andrew wa shule ya msingi Nambunga. Wengine ni Jamilu Manzi, Omary Selemani, Ziada Twalibu, Siamini Dadi, Zaituni Ismaili na Udhaifu Issa, huku ndugu Hamisi Mussa wa kijiji cha Mnanje akitarajia kupokea baiskeli yake kutokana na makubaliano ya kikao kilichopita cha kamati hiyo.
Aidha kamati imewataka watu wote wanaohusika na kuratibu fedha hizo, kuhakikisha akaunti zao za benki zinafanyakazi huku ikitaadharisha juu ya matumizi mabaya na kuahidi kuitembelea miradi hiyo ili kujiridhisha kwenye hatua za utekelezaji wake.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa