Mkuu wa Wilaya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya amewataka maafisa ugani kuwa mfano wa wakulima kwa kuwa mstari mbele katika kuhamasisha shughuli za kilimo vijijini na kuacha tabia ya kukaa ofisini.
Ameyasema hayo Februari 27, 2023 katika hafla ya ugawaji pikipiki 50 kwa maafisa hao wilayani ya Newala zilitolewa na Serikali kupitia wizara ya kilimo iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Newala.
Katika nasaha zake Mkuu huyo wa wilaya amesema Serikali imeshatekeleza wajibu wake wa kutaka kulifikia lengo la kuinua kilimo kwa kujibu changamoto ya usafiri hivyo ni wakati wa maafisa hao kuthibitisha utaalamu wao kwa kuwa karibu na wakulima katika kuinua kilimo.
Aidha amewasisitiza kuwa nia ya dhati inahitajika katika utendaji wao kwa kuwa jamii kubwa ya wakulima wa Newala ni wale wanaoamini katika kilimo cha mazoea na kinachotakiwa sasa ni kubadilisha mtazamo huo walionao kwa vitendo na sio maneno.
Kwa upande wake Mkuu wa idarq ya kilimo Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Calistus Komba ameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao, huku akiwataka wakulima kujitokeza kuwatumia maafisa kikamilifu kwa kuwa sasa hakuna changamoto ya kufika mashambani.
Bi. Hawa Yusuph afisa ugani wa kata ya Mtopwa halmashauri ya Wilaya ya Newala na Bwn. Hassan Haji Afisa Ugani wa Kata ya Mkulung'ulu Halmashauri ya Mji Newala wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa pikipiki hizo huku akiahidi kuongeza ufanisi katika kuinua kilimo chenye tija.
Wilaya ya Newala ina jumla ya maafisa ugani 56 na sita kati yao waliopeka pikipiki mpya hivi karibuni na katika mgao huu Halamashauri ya Mji Newala imepata pikipiki 22 na Halmashauri ya Wilaya Newala imepokea pikipiki 28.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa