Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kushiriki uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019, kwa kujiandikisha, kupiga kura pamoja na kuwania nafasi ya mwenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji.
Ameyasema hayo mwishoni mwa juma lililopita akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Newala ya kuongea wa watumishi wa umma, madiwadni, wakandarasi na wafanyabiashara kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na kampeni aliyoianzisha ya Shule ni Choo.
Mhe. Byakanwa amesema uchaguzi huo ni wa kitaifa na litaanza zoezi la kujiandisha kwenye daftari la mpiga kura, kwa kila mtanzania mwenye akili timamu na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea kujiandikisha kwenye kitogoji chake, kuanzia tarehe 08/10/2019 hadi 14/10/2019, na kufuatia na uchaguzi wenyewe utaofanyika tarehe 24/11/2019.
Mkuu wa mkoa amewataka madiwani, maafisa watendaji kufanya mikutano na wananchi kuwaelimisha juu ya umuhimu wa uchaguzi huo kwa na kuwahamasisha watu wenye umri wa miaka 21 na kuendelea wenye sifa za kuwa viongozi bora wajitokeza kuwania nafasi hizo katika maeneo yao bila kubagua jinsi zao.
Sambamba na hilo Mkuu wa mkoa pia ameendelea kuhamasisha kampeni yake ya shule ni Choo kwa wananchi, viongozi, taasisi binafsi na za umma kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu vyoo vya waalimu na wanafunzi kwenye shule zenye mapungufu baada ya kubaini upungufu huo mashuleni.
Aidha amesema wakurugenzi wanalo jukumu la kuhakikisha wanabuni mbinu na mipango mingine ya kufanikisha mpango huo na kama wananchi wataamua kuwekeza kwenye mambo madogo madogo, upo uwezekana wa nchi kupiga hatua kubwa ya maendeleo waliyosababishwa na wananchi wenyewe.
Katika kikao chake na wakurugenzi, watumishi wa serikali, wakuu wa taasisi na madiwani kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya Newala, ilifanyika harambee ya kampeni hiyo ambapo kwa pamoja jumla ya mifuko ya saruji 679 iliahidiwa na fedha Tsh.8,250,000/= ziliahidiwa.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Newala, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo, amesema watayazingatia maagizo ya kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi hasa wa vijijini pamoja na kuunga mkono kapeni ya Shule ni Choo kwa vitendo.
Kampeni ya Shule ni Choo mkoani Mtwara imeanzishwa na Mkuu wa mkoa baada ya kubaini uhaba vyoo na vyoo visivyo salama na rafiki kwa matumizi ya waalimu na wanafunzi wawapo shuleni, na kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12/10/2019 na Rais Mstahafu awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akimbatana na waziri wa afya na waziri wa elimu
Kauli mbiu yake ni “Changia Sasa ili Uweze Kumsitiri Mwalimu na Mwanafunzi Wakiwa Mazingira ya Shule.” mtu aneweza kuchangia fedha, malighafi watakayowezesha kufanikisha ujenzi wa vyoo hivyo au kujenga choo chenyewe.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa