Mkuu wa Wilaya Newala Mhe. Mwangi Kundya amewataka wataalam wa mausala ya kilimo na fedha kuwaelimisha wakulima juu ya utunzaji na matumizi bora ya fedha wanazozipata baada ya kuuza mazao yao.
Mhe. Kundya ametoa wito huo wakati anaongea na wajumbe wa mkutano wa baraza la madiwani la robo ya nne 2024/2025 la halmashauri ya Mji Newala ambapo amewataka kuwasaidia wakuliwa kupata uwelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na matumizi ya fedha.
“Tunawasihi wataalamu wetu wa kilimo watekeleze wajibu wao lakini iko haja ya wataalamu wetu wa fedha kuelimisha jamii yetu hapa panahitaji namna bora ya kufanya hali ya maisha ya wakulima yabadilike”
Hata hivyo Mkuu wa wilaya amewataka wataalam wa halmashauri kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa wao ndio waliobeba dira ya maendeleo ya wananchi kupitia uwajibikaji na usimamizi.
“Mheshimiwa mwenyekiti wananchi wanataka maendeleo maendeleo hayana muda yahitajika kila siku, kila wakati na kila mahali hivyo katika kipindi hiki maalum cha uendeshaji shughuli za halmashauri thamana ya kuhakikisha maendeleo kwa mwananchi yanendelea kupatikana yapo kwenye mikono yenu”.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye amesema wamepokea maagizo hayo ambayo tayari walishaanza kuyafanyia kazi.
“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya sisi tayari tilishaanza ndio maana umeona katika kuwasilisha taarifa za kata uliona wakuu wa Idara na vitengo wakiwasilisha kwa kuwa hao ndio walezi wa hizo kata na kila kitu wanakielewa na kushiriki huu ni muendelezo tu”.
Mkutano huo umefanyika Agosti 18, 2025 katika ukumbi wa halmashauri ya Mji Newala ulikuwa unajadili shughuli za maendeleo zilizotekelezwa katika kipindi cha Aprili-Juni 2025 ambapo mpaka kufikia Juni 30 halmashauri imetekeleza miradi yenye jumla ya shilingi bilioni 7.26.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa