Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala ndg. Andrew Mgaya, amewataka wakuu wa vituo vya Afya, waratibu wa mfuko wa afya ya jamii uliboreshwa (ICHF) na Chanjo ya Surua-Rubella, kushirikiana na maofisa watendaji wa kata na maafisa Tehama, kuboresha huduma zao ili kufikia lengo kusudiwa la Serikali.
Mkurugenzi Mgaya ameyaeleza hayo leo Jumatatu 16/09/2019, alipokutana na wataalamu hao kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri, cha kujadili mbinu na kupeana uzoefu wa kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi na kufanikisha malengo tarajiwa.
Amesema ili kazi yoyoye ilete mafanikio hakuna budi kuwe na mshikamano wa pamoja na kwenye ngazi ya halmashauri watendaji wa kata ndio wenyenguvu wa kuratibu shughuli zote hivyo uzajili wa CHF iliyoboreshwa na chanjo ya Surua-Rubella ni lazima wawe kwenye nafasi ya uratibu wa zoezi hilo.
“Maagizo haya ni ya serikali na ni yakitaifa hivyo ni lazima tuyatekeleze hakuna namna, hawa watendaji ndio mabosi wenu huko unakofanya kazi, sasa kuanzia sasa ni lazima wawe sehemu ya utekelezaji hasa kwenye ICHF, na ninataka kuanzia leo liundwe group la whatsapp na wao wakiwemo, na wote niliowaita hapa mtatao mrejesho wa kile mnachokifanya kila siku, ili tuone mmefanikiwa wapi na mmekwana wapi ili tushauriane na kupeana uzoefu.” amesisitiza Mgaya.
Hata hivyo Mkurugenzi Mgaya amewataka wataalamu hao kutambua kuwa mfanikio yanatokana na ubunifu wa kiutendaji na hakuna njia yamkato, hivyo huu niwakati wakutumia maarifa waliyonayo kufanikisha mipango ya serikali wanayoitumikia na wananchi ambao ndio walengwa wakuu.
Aidha amewataka wakuu wa vituo vya afya kuzingatia maadili ya kazi, kutunza kumbukumbu zote za mapato na matumizi ya fedha pamoja na dawa, kwani hoja yoyote itakayoibuka muhusika atalazimika kuijibia mwenyewe huku akiwasisitiza kufunga mifumo ya kukusanya fedha (GOT-HOMIS) kwenye vituo vyao kama serikali ilivyoelekeza.
Kwa upande wake mratibu wa CHF iliyoboreshwa wa halmashauri hiyo Bi. Grace Mtulo amesema kutokana na kikao cha leo, anayomatumani makubwa ya kuongeza kasi ya usajili ya kaya kwa kuwa timu imeongezeka, na kwa wale wataoonekana kuwa wazito kwenye zoezi hilo watawekwa pembeni hivyo ameomba uwepo wa ushirikino baina yao.
Naye mratibu wa chanjo halmashauri ya Mji Newala Bi. Marium Shabani, amesema sasahivi wapo kwenye kampeni ya kitaifa yakutoa chajo ya Surua-Rubella inawahusu watoto kuanzia miezi 9 hadi miaka 4 na miezi 11 na chanjo ya polio kwa watoto wa mwaka 1.5 hadi miaka 3.5 zoezi litakaloanza tarehe 26/09/2019 mpaka tarehe 30/09/2019.
Bi. Marium ameitaka jamii kuhamasishana na kujitokeza kupata chanjo hizo, na leongo ni kuwafikia ambao hawajapata kabisa na wale ambao hawajapata kikamilifu kwani kitaifa inaonyesha mpaka sasa waliopata ni 85% huku lengo likiwa ni 100%, na kuongeza kuwa magonjwa hayo hayana tiba, tiba yake ni kinga ambazo ni hizo chanjo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa