Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye amewapongeza wataalam wa afya na lishe pamoja na watendaji wa kata kwa utekelezaji nzuri wa afua za lishe na kuwataka kugeukia masuala ya usafi.
Mkurugenzi Nnauye ameyasema hayo katika kikao cha robo ya nne 2024/2025 cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi kata, ambapo ameeleza kuwa tathmini kuhusu lishe kata zote vimefikia vigezo na kufanya vizuri.
“Kama tulivyotoka huku kwenye score card ya lishe yote ikawa ya kijani, tumeanza mwaka mpya wa fedha hii julai, jukumu letu la usafi Pamoja na vyoo bora yanaanza lakini sasa tusibweteke ili tusirudi nyuma kwenyemambo yote” Amesisitiza Mkurugenzi
Katika hatua nyingine katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu amewataka wajumbe wa kikao hicho kuwa chachu ya uwepo wa amani na utulivu katika maeno yao kwa kuripoti viashiria vya uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake kaimu katibu tawala wa wilaya ya Newala Bi. Mary Twamgabo amefurahishwa na hali ya lishe huku akisititiza elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi iwe ya kudumu kwa kutumia mbinu mbalimbali mpaka jamii ipate uelewa.
“Kuhusu vyoo bora hilo lisiwe sehemu ya kutukatishe tamaa, sisi tuendelee kuwaelimisha na tusisubiri wakati wa mikutano moja moja, kupitia nyumba kwa nyumba, kupitia watoa huduma ngazi ya jamii mwisho wa siku naamini tutafanya vizuri”. Ameeeleza Twamgabo
Afisa afya mazingira wa halmashauri hiyo Ndg. Jackson Lumeya amefafanua hali ya usafi inazidi kuimarika baada ya kuanza kutekeleza kampeni ya kuboresha hali ya usafi wa mazingira Pamoja na ujenzi wa vyoo bora katika robo ya tatu 2024/2025mbapo
Ndg. Lumeya amesema “Tunachoomba ni ushirikiano kwa wananchi na watendaji ili tuweze kufikia malengo ya serikali ya hali ya usafi na tuweze kufikia 100%”
Hata hivyo Lumeya amebainisha kuwa kwasasa hali ujenzi wa vyoo imefikia 59% toka 38% iliyokuwepo wakati wanaanza utekelezaji na kaya zenye usafi wa mazingira 47% toka asilimia 26 ya awali.
Kutokana na taarifa ya hali ya usafi kupitia kikao cha afya ya msingi kubaini kutokuwa na hali ya kuridhisha ya usafi kilifanya uamuzi wa kupata taarifa ya hali ya usafi kwenye kaya na ujenzi wa vyoo bora ya kila robo kupitia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya kata.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa