Mkurugenzi wa halamshauri ya mji Newala, ndugu Andrew Mgaya leo Ijumaa Mei 24, 2019 amezindua rasmi zoezi la uandikishaji wanachama wa Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa kwa kukabidhi simu na vifaa vingine kwa maafisa waandikishaji 59 wa mitaa na vijiji wa halmashauri.
Mkurugenzi Mgaya amekabidhi vifaa hivyo kwenye ukumbi wa mikutano wa hospatali ya wilaya Newala, ambapo amewakata maafisa hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwa kutembelea na kuzihamasisha kaya, vikundi vya jamii na taasisi mbalimbali ikiwemo shule ili wajiandikishe na kuifikia adhma ya serikali ya kuwafikishia wananchi huduma bora za afya kupitia CHF iliyoboresha.
Aidha katika kutoa motisha kwa maafisa hao amewaahidi kutoa shilingi laki moja (Tsh. 100,000/=) kwa afisa atakaefakiniwa kusajili kaya nyingi, kwa kufikisha zaidi ya asilimia 80 ya usajili kwenye maeneo yao na kuwataka kulichukulia jambo hilo kuwa ni fursa kwao.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewasihi maafisa hao kuwa waadilifu kaika utendaji kazi wao na ameshauri fedha wanazokusanya ni vema wapeleka kwenye akaunti za bank kila wanapofanya usajili kwani hiyo itasaidia kuondokana na tamaa ya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Katika hatua nyingine amewata wananchi wawatambue maafisa hao na kuwapa ushirikiano ikiwa pamoja na kujiunga kwa wingi kwani CHF iliyoboreshwa ndiyo suluhisho la matibabu hasa kwa wananchi wa kipato cha kawaida na ni muhimu kwao kujiunga.
Kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa wa halmshauri hiyo Bi. Grace Mtulo amewataka maafisa hao kuwa mfano kwa jamii kwa wao wenyewe kuanza kujisajili kwenye mfuko huo na kufanya uhamasishaji kwa wananchi wengine.
Aidha Bi. Mtulo amefafanua kuwa zoezi hilo ni fursa ya kujiongezea kipato kwa maafisa waandikishaji, kwani ukisajili kaya moja wenye watu 6 gharama yake ni shilingi elfu thelethini (30,000/=) na asilimia kumi (10%) itarejeshwa kwa muandikishaji.
Sambamba na hilo amevitaja vifaa walivyokabidhiwa kuwa ni Simu 59, vitambulisho, Pochi za kuwekea vitambulisho pamoja na fomu za usajili wananchama huku akiwataka maafisa hao watumie vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa na sio kwa mambo yao binafsi.
Hata hivyo Mtulo ameeleza kuwa zipo faida nyingi za kujiunga na CHF iliyoboreshwa, na baadhi ni kaya iliyoandikishwa wenye watu 6 kutibiwa mwaka mmoja bure, kupata huduma kwenye kituo chochote cha afya cha serikali ndani ya mkoa, huduma ya kulaza wagonjwa, upimaji, upasuaji mdogo na ongezeko la dawa.
Wakizungumza kwa niaba ya maafisa wengine waandikishaji Bwana Awadhi Uleme kutoka Mnalale, Bi. Salama Hashimu wa Mkoma 1 na Abdulatifu Halifa kutoka mtaa wa Juhudi-Makonga wamesema wapo tayari kwenda kutekeleza jukumu hilo kwa kuwa mafunzo ya kutekeleza kazi hiyo walishayapata mapema tangu mwezi februari mwaka huu na hatua hiyo itaenda kuwarahisihia kazi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa