Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara Andrew Mgaya, amesema halmashauri yake imeweka mikakati ya kuongeza mapato yake ya ndani kwa kuanzisha vyanzo vipya ya ukusanyaji.
Hayo ameyaeleza jana, Alhamis december 06, 2018 kwenye kikao cha Ushauri wa Maendeleo wilaya ya Newala (DCC), kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya Newala.
Mgaya amesema halmashauri yake imeshachukua hatua za kukabiliana na ufinyu wa mapato na kuacha kutegemea mapato ya serikali kuu na ushuru wa zao la korosho pekee, na kuongeza kuwa baadhi ya vyanzo hivyo tayari vimeshaanza kuonyesha mafanikio.
Amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na upimaji shirikishi wa viwanja zaidi ya 300, kuongeza mabucha ya nyama hadi kufikia 10 ndani ya soko kuu, kusimamia tozo za usafi wa mazingira, kuanzisha chumba cha kuifadhia mizigo ndani ya soko, kuanzisha eneo la kushusha mizigo (bandari kavu) na ujenzi wa mabanda 100 biashara.
Mgaya amevitaja vyanzo vingine kuwa, ni hivi karibuni kuanza kutumia mashine ya kuchunguza mwili mzima (full blood picture) kwenye hospitali ya halmashauri, kuanza kutumika kwa zahanati nne na kituo kimoja cha afya pamoja na ujenzi wa mabanda ya biashara karibu na eneo la hospitali.
Hata hivyo Mkurugenzi Mgaya, ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya Mhe. Aziza Mangosongo, ambaye amewataka wakugenzi kukaa na wakuu wa idara kujadili na kuibua vyanzo vipya vya mapato pamoja na kuwawekea maafisa watendaji malengo ya ukusanyaji kwa kila mwezi.
Aidha katika hatua nyingine, kutokana na Mamlaka ya Mapato (TRA) wilayani hapa kuotofanya vizuri kwenye kukusanya kodi za majengo na mabango, Mkurugenzi huyo ameishauri taasisi hiyo kukutana na wataalamu wa halmashauri ili kujifunza mbinu walizokuwa wanazitumia kwenye zoezi hilo.
Taarifa ya TRA ya ukusanyaji kodi 2017/2018 imeonyesha mapato yameshuka kwani kwa halmashauri ya Mji Newala walikadiria kukusanya milioni 40 kwenye majengo lakini hawakufikia lengo kwa kukusanya milioni 26,320,000/- pekee, kiwango ambacho ni tofauti na awali kwani halmashauri ilikuwa inakusanya zaidi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa