Hospitali ya wilaya Newala iliyo chini ya Halmashauri ya Mji Newala imepokea msaada shuka za wagonjwa 100 kama msaada kutoka taasisi inayojishughulisha na uuzaji dawa za binadamu ya Mkuti Phamacy.
Msaada umetolewa jana Jumamosi Tarehe 4/12/2021 kwenye mkutano wa kuitimisha ziara ya mbunge wa jimbo la Newala mjini Mhe. George Mkuchika uliofanyika katika viwanja wa mahakama ya mwanzo Newala mjini, ambapo mwakilishi wa taasisi hiyo Bi. Mwanaidi Mtego amesema mssada huo utasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa shuka katika hospitali hiyo.
Aidha Bi. Mtego amefafanua kuwa wao kama wadau wamaendeleo wamekuwa wakifanya kazi na serikali kupitia wizara ya afya katika kusaidia hospitali mbalimbali zenye uhitaji kwa kile wanachokiweza kusaidia “Ndugu muheshimiwa mbunge na waziri hii si mara yetu ya kwanza kutoa msaada, tumeshatoa mashuka 200 hospitali ya Mkomaindo Masasi na pamoja na kutoa shuku hizi 100 hospitali ya wilaya Newala lakini tutaenda kukabidhi shuka zingine 100 kituo cha Afya Kitangali” alisema.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi wa Newala Mbunge wa Newala Mhe. George Mkuchika ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa kuiga mfano wa Mkuti Phamacy katika kujitoa kuisaidia jamii hasa kwenye maeneo muhimu kama hospitali, shule na maeneo yanayoigusa jamii.
Aidha Mhe. Mkuchika ameishukuru taasisisi hiyo kwa uzalendo wao wa kujitoa kuchangia maendeleo ya wananewala kwa kuwa bado maeneo mengi ya kitaasisi na kiidara yanahitaji kuongezewa nguvu na pale wanapojitokeza wadau kusaidia inachochea ustawi wa jamii.
Mara baada ya kupokea msaada huo wa mashuka alikabidhi kwa mganga Mkuu wa halamshauri ya mji Newala Dkt. Joseph Fwoma amabaye alimshukuru mbunge kwa kuwajali wananchi na kuwatafutia misaada inayowanufaisha watu wote hasa kwa upande wa afya kwa kuwa sekta hiyo ina mahitaji mengi ya kila siku.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa