Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, ametoa pongezi kwa idara ya elimu halamshauri ya Mji Newala kwa jitahadi kubwa za mipango ya kuongeza ufulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha pili.
Ameyazungumza hayo leo asubuhi Jumatano January 29, 2020 mjini Newala wakati anaongea na wananchi kupitia Redio Newala Fm, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani hapa ambapo ameeleza kuwa ameridhishwa na jitihada zinazooneshwa na waalimu mashuleni.
Mhe. Byakanwa amesema ameridhishwa zaidi na jitihada za shule ya sekondari Malegesi ambayo miaka miwili nyuma ilikua moja ya shule zilifanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha pili lakini matokeo ya mwaka huu yamekua mazuri na hiyo inaonyesha namna gani watu wanatakiwa kuwajibika na kuleta maendeleo.
Aidha amepongeza msimamizi nzuri wa kampeni ya shule ni choo kwa hapa wilayani Newalana kueleza kuwa wilaya ya Newala ni mfano wa kuigwa kwa muitikio nzuri na kutoa pongezi kwa Mkuu wa wilaya Mhe. Aziza Mangosongo kwa usimamizi wa kampeni hiyo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa agizo kwa Maofisa watendaji wa Kata kuwakamata wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao waliofaulu kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali kwa mwaka huu, ili wafikishwe mahakamani kwa hatua zingine za kisheria.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa