Mkuu wa Mkoa Mtwara Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa amemaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi waliotoa maeneo yao kujenga shule ya sekondari Dr. Alex Mtavala na halmashauri ya mji Newala, huku akielekeza kuwa hakuna mwananchi atakayelipwa fidia na serikali mkoani Mtwara, kwakutoa kipande cha ardhi yake kuchangia miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi wenyewe.
Mhe. Byakanwa ameyazungumza hayo mwishoni mwa wiki iliyopita siku Ijumaa 20/09/2019 akiwa katika ziara yake wilayani Newala ya kutatua migogoro ya ardhi, wakati anaongea na pande hizo mbili, ambapo wananchi hao kupitia mwenyekiti wao Said Ibrahim Uledi na katibu wa malalamiko Lezle Chikolo, walikuwa wanailalamikia halmashauri hiyo kutowalipa fidia ya maeneo yao.
Amesema kumekua na tabia mbaya imeanza kujitokeza miongoni mwa wananchi ambao walitoa ardhi yao kwa ajili ya shughuli za maendeleo na baadae wanapoona ukuaji wa miji na maeneo hayo waanza kuibua migogoro ya kudai fidia kwa tama ya fedha, na hata eneo hilo liliibuliwa kwenye ngazi ya kata hivyo kama ni malipo wangekubailiana kwenye vikao vya awali ngazi ya kata au kijiji na malipo yafanyike huko na huo sio mgogoro, shule hiyo na maeneo yake ni mali ya serikali.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa amesema inashangaza kuona viongozi wa walalamikaji, walikua viongozi wakati wa mchato wa kuanzisha shule hiyo, ndg. Said Uledi alikua mweyekiti wa kijiji na Lezle Chikolo alikua Mratibu Elimu Kata wa kata hiyo na wenyewe wanakiri kushiriki na kuhamashisha ujenzi wa shule hiyo na sasa wanageuka kama walikua hawajua kitu chochote.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kujitolea ardhi yao kwa ajili ya kuwezesha maendeleo katika maeneo yao, kwani serikali inandelea kutekeleza miradi iliyoanzishwa na wananchi kama zahanati, shule na miradi mingine lakini makubaliano yote yafanyike kwenye ngazi inayofanyika uibuaji wa miradi hiyo na sio kungoja mradi umeshatekelezwa ndio unaanza kuibua sintofahamu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ndg. Andrew Mgaya, amekiri kufikiwa na malalamiko ya wananchi hao, lakini amesema aliwajibu kwa maandishi kuwa suala hilo wakalimalize kwenye ngazi ya kata, kwani wao wenyewe ndio waliuanzisha mradi huo na serikali kupitia halmashauri waliukamilisha kama muongozo wa mwaka 2005 wa utekelezaji wa miradi ya maendele unavyoelekeza.
Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi, amesema wananchi hao sio wa kweli kwa kuwa tangu shule hiyo inaanzishwa mwaka 2006 na shule zingine zote za kata zilizoanzishwa wakati huo wilayani Newala, hazikuwa na migogoro yoyote zaidi ya mgogoro mmoja katika kata ya Mcholi 1, vijiji vikigombania shule hiyo ijengwe kwenye kijiji chake lakini wananchi waliridhia kutoa maeneo yao.
Shule ya sekondari ya Dr. Alex Mtavala ipo mtaa wa Legeza kata ya Julia halmashauri ya Mji Newala, mchakato wa kuanzishwa kwake ulianza mwaka 2006 eneo hilo likiwa kata ya Luchingu na kusajiliwa rasmi mwaka 2008.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa