Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti leo Ijumaa 12 Disemba, 2021 amepokea madarasa ya 19 ya shule za sekondari halmashauri ya mji Newala, yenye thamani ya shilingi milioni 380 yaliyojengwa kwa mpango maalumu wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa dhidi ya UVIKO-19.
Akiongea na wanachi katika viwanja vya shule ya sekondari Newala mara baada ya kupokea madarasa hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Newala, Brigedia Gaguti amesema amefurahishwa kwa namna mradi huo ulivyotekelezwa kwa uwazi na haraka kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Aidha ameshauri utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo utumie utaratibu uliotumika kutekeleza mradi huu ili upatikane usimamizi wa wa pamoja kwa kuzingatia thamani ya fedha na ukumilishaji wa miradi kwa wakati pasipokuwa na ubabaishaji.
Hata hivyo Mkuu Mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuupatia Mkoa shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi ya ujenzi wa madarasa 452 ya mpango maalam wa UVIKO-19 pamoja na fedha zingine shilingi bilioni 22 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 2021/2022.
Kutokana na kukamilika kwa mradi huo Brigedia Gaguti amesema mkoa sasa upo tayari kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo unaoanzia Januari 2022 na shule zihakikishe zinakamilisha zoezi la uwekaji wa dawati kwa muda uliobaki.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya, amesema halmashauri ya Mji Newala na wilaya kwa ujumla imekamilisha utekelezaji wa mradi huo wa madarasa na kuwataka wasimamizi wa shule na wanafunzi kuyatunza madarasa hayo.
Naye Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Daud Mwariko ameupongeza uongozi wa mkoa kwa kuweka utaratibu nzuri ya kutekeleza mradi huo, uliopelekea kukamilisha ujenzi wa madarasa kama ili kusudiwa na kwa muda muafaka.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa