Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Marco Gaguti ametoa zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 120 yakiwemo magari, pikipiki, baiskeli, vyeti na fedha taslimu kwa wadau wa elimu waliofanya vizuri kwa mwaka 2021.
Brigedia Gaguti amatoa zawadi hizo jana Jumatano Aprili 06, 2022 kwenye kilele cha sherehe za juma la elimu kimkoa zilizofanyika katika viwanja vya sabasaba halmashauri ya mji Newala, ambapo ameeleza kuwa zawadi hizo ni motisha ya kuongeza hari kazi kwa walimu, wanafunzi, shule na halmashauri kwa ujumla.
Akihutubia wananchi na wadau wa elimu waliohudhuria shererhe hizo kutoka halmashauri zote 9 za mkoa wa Mtwara amesema mkoa umedhamiria na kuweka mikakati ya kuinua kiwango cha ufaulu ili kuondoa dhana ilijengeka kuwa Mkoa wa Mtwara ni kati ya mikoa dhaifu kwa ufaulu katika matokeo ya kitaifa na kuwa na kiwango cha chini cha elimu.
Akieleza kuhusu mikakati iliyopo Mkuu wa mkoa amesema tayari mkoa na serikali umeshachukua hatua ya kuandaa juma la elimu na kutoa zawadi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hivyo wazazi, walimu na wanafunzi kila mmoja unapaswa kuwajibika ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Maadhimisho ya Juma la Elimu mkoani mwaka huu 2022 yamebeka kaulimbiu isemayo "Tuwajibike Pamoja Kuleta Maendeleo Ya Elimu Mtwara"
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa