Katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru Tanzania, Serikali imedhamiria kupambana kikamilifu na ujinga , maradhi pamoja na umasikini kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu kuanzia awali mpaka chuo kikuu ili kuondokana na kizazi cha utumwa.
Mkuu wa wilaya ya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya ameyasema hayo kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Tarehe 9 Disemba , 2021 yaliyoandaliwa na halmashauri ya mji Newala na kufanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Newala mjini.
Alhaj Kundya amesema huu sii wakati wa utumwa wa kifikra hivyo wazazi wanatakiwa kuhimiza watoto wao kuwa na juhudi kubwa katika elimu kwa kuwa serikali ya awamu ya sita tayari imeipatia wilaya ya Newala zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa madawati 58 na fedha zingine milioni 940 za kujenga shule mbili mpya.
Aidha Alhaj kundya amefafanua kuwa dunia sasa ipo wakati wa matumizi ya teknolojia na msingi wake ni elimu, hivyo wazazi waache kuwachelewesha watoto wao kwenye ngoma za asili na kuokota korosho kwa kuwa kufanya hivyo ni kuliandaa taifa la watumwa kwasababu ya kukosa maarifa yanayohitajika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala Bi. Shamim Mwariko amesema katika kuadhimisha siku hiyo muhimu halmashauri iliona vema maadhimisho yajikite kwenye kuhamasisha mambo ya afya kutoa uelewa, kupima pamoja na kutoa matibabu kwa hiyo hiyo itakuwa njia moja wapo ya kuhamasisha wananchi kuzingatia huduma za afya.
Katika hatua nyingine Bi. Mwariko ameeleza kuwa afya ni rafiki wa amaendeleo na ili Tanzania yenye uchumi ulioimarika ipatikane ni lazima afya za watu wake nazo ziwe imara na hatua ya muhimu na yakwanza ni kufanya uchunguzi wa afya mapema.
Akisoma taarifa ya hospitali ya wialaya ya Newala Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Newala Dkt. Joseph Fwoma amesema hali ya utoaji huduma hospitalini hapo imeimarika serikali imefanya maboresho ya miundombinu, vifaa tiba pamoja na upatikanaji wa dawa changamoto iliyopo ni wananwake kutojitokeza kupima saratani ya shingo la kizazi, tatizo linao onekana kushamiri kwa wananwake wengi wa eneo hilo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa