Mkuu wa wilaya Newala Alhaj Mwangi Rajabu Kundya leo Jumamosi Tarehe Novemba 27, 2021 amezindua Zahanati ya Amani iliyopo ya kijiji cha Amani, Kata ya Mcholi I halmashauri ya mji Newala, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watoa huduma.
Alhaj Kundya amesema, dhamira ya serikali ni kuwatumikia wananchi wake kwa kuwapatia huduma bora zenye ustawi kwa jamii yote kama ilivyojimbambanua kwenye mipango wake mbalimbali na ndio maana ipo mstari wa mbele katika kujenga miundombinu muhimu katika sekta zote.
Kundya amebainisha kuwa afya ndio ustawi wa maisha ya mwanadamu na kupatikana kwa zahanati hiyo ni hatua ya kuokoa maisha ya wananchi kutokana na maradhi hivyo wakazi wa eneo hilo washirikiane na wafanyakazi wa kituoni hicho katika kufanikisha utoaji na upatikanji wa huduma bora za afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halamashauri hiyo Bi. Shamim Daudi Mwariko amesema halmashauri kazi yake ni kusimamai ukutekelezaji wa mipango ya serikali ambayo imelenga kupeleka huduma zote muhimu karibu na wananchi wenyewe na ndio maana kazi hiyo imesimamiwa kikamilifu na halmashauri.
Hata hivyo Mwariko amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Mhe. George Mkuchika kwa kuwatafuta wadau wamaendeleo kutoka Nchini Japan waliotoa fedha shilingi milioni 139.5 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo na fedha zingine kama hizo kujenga zahanati ya Mahumbika amabayo nayo tayari imeshaanza kufanya kazi.
Diwani wa Kata hiyo Mhe. Maarufu Chakane amesema, kuzinduliwa kwa zahanati hiyo ni furaha ya aina yake kwa wakazi wa Kata hiyo yenye vijiji vya Amani, Pachoto, Mnalale, Chiunjila na Chikwedu ambao awali walikua wanapata huduma za afya kwenye Kata jirani za Mkunya na Mcholi II lakini kwasasa uwepo wa zahanati hiyo ni ukombozi kwao.
Akiongea kwa niaba ya wananchi Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw. Athumani Mkuka wamesema wanaishukuru serikali na idara zake zote kutokana na jambo hilo kubwa ambalo kwao ni sherehe, huku akisisitiza kutoa ushirikiano kwa watumishi na ulinzi wa miundombinu ya zahanati.
Aidha katika siku hiyo ya uzindizi wananchi walishiriki katika ujenzi wa nyumba ya Mganga wa Zahanati itakayogharimu shilingi milioni 36, milioni 6 ikiwa ni thamani ya nguvu za kujitolea toka kwa wananchi na milioni 30 ni fedha za mapato ya halmashauri huku mwananchi mmoja ajitolea nyumba yake kwa ajili ya kuishi mganga mpaka ujenzi utakapo kamilika.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa