Halmashauri ya mji Newala mkoani Mtwara hadi kufikia Machi 31, 2019, imetumia shilingi bilioni 2.28 kutekeleza miradi ya maendeleo fedha ambazo ni sehemu ya shilingi bilioni 2.29 ilizopokea kutekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 4.81 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Hayo yameelezwa kwenye kikao cha baraza la Madiwani la halamashauri hiyo cha robo ya ya tatu kilichofanyika Machi 3 na 6 2019, katika ukumbu wake wa mikutuno mjini Newala ambapo imeelezwa kuwa shilingi bilioni 1.47 ni fedha zilizopokelewa mwaka wa fedha 2018/2019 na shilingi milioni 807 ni fedha za bakaa ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Aidha makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Othuman Bilali amewaomba madiwani kushirikiana na watendaji wa serikali kusimamia, kuhimiza na kuwaelimisha wananchi juu ya ulipaji wa tozo mbalimbali za kisheria kwani hali ya mapato ya ndani ni mbaya hivyo nguvu ya pamoja ya ukusanyaji mapato inahitajika ili halmashauri iweze kujiendesha.
Aidha katika hatua nyingine amesema hamlamashauri imepokea kwa mikono miwili taarifa ya kupata hati safi na kuahidi kuendelea kuwasimamaia wataalam katika kutekeleza shughuli za miradi ya maendeleo kwa kufuata taratibu zinazokubalika na kwa uadilifu ili kuitetea hati hiyo kwa mara nyingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halamashauri Ndg. Andrew Mgaya amefafanua kuwa hali ya mapato ya ndani hairidhishi hivyo amewaomba madiwani kusaidia kutoa uelewa kwa wananchi wao kusuhu vyanzo vipya vya mapato vilivyoanishwa hasa anuwani za makazi na vibali vya ujenzi ambapo kwa sasa kila mwananchi enayefanya ujenzi kwenye eneo lake ni lazima awe amelipia kibali.
Mgaya amefafanua kuwa vibali hivyo vya ujenzi vinatolewa kwa mtu yoyote anayeendeleza ardhi yake kwa kufanya ujenzi katika eneo lote la halmashauri ya mji, na kwa kufanya hivyo itasaidia kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na ujenzi holela pamoja na kusimamia sheria za mipango miji.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa wilaya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amewata madiwani kutambua ajenda ya mapato ndio ajenda kuu katika halmashauri kwani bila mapato hakuna halmashauri na hata takwimu za sasa za kitaifa zimeonyesha halmashauri ipo nafasi ya 157 kati ya halamshauri 185 hivyo jitihadi zaidi zinaitajika kuongeza ukusanyaji.
Mhe. Mangosongo pia amesema suala la vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ni la kitaifa hivyo kila mmoja aone umuhimu wa kuwahimiza walengwa kujitokeza kuchukua vitambulisho hivyo kwani baada ya kumaliza kuuza vitambulisho elfu 5 vya awamu ya kwanza, awamu ya pili wilaya imepewa vitambulisho elfu 13 na vilivyouzwa hadi sasa havijafika elfu 5.
Sambamba na hilo Mkuu wa wilaya ameipongeza halmashauri kwa kupata hati safi na kushika nafasi ya kwanza kimkoa nafasi ya 4 kikanda na ya 6 kitaifa katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018, na kuitaka halmashauri kuendeleza utendaji bora wa kazi ili kuzitetea nafasi hizo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa