Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Newala hasa wanaoishi maeneo yanayozunguka Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara, kuwa walinzi miundombinu ya chuo ili kuleta maendeleo kusudiwa kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Mhe. Rais Magufuli ameyazungumza hayo jana Jumatano Tarehe 03 Aprili, 2019, alipokuwa anaongea na wananchi katika hafla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa upanuzi na ukarabati miundombinu ya chuo hicho chini ya ufadhili wa serikali ya Canada.
Amesema kama wananchi wataiunza miundombinu hiyo vizuri, italeta manufaa ya muda mrefu kwa wakazi wa Mtwara na nchi kwa ujumla “lakini ndugu zangu wa Newala, serikali ya awamu ya tano imesha jipambanaua katika shughuli zake, hakuna mtu alitegemea majengo yaliyokuwa yanaanguka hapa sasa yakaonekana katika hali hii.. Hayo ni malipo halali kwa kura zenu, hayo ni malipo halali kwa maendeleo tuliyoyaahidi kuwatimizia wananchi”, napenda muamini serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake”. Alifafanua Rais Magufuli.
Aidha Rais Dkt. Magufuli ameipongeza wizara ya elimu kwa usimamizi nzuri fedha za serikali na wafadhili wakati wa utekelezaji wa mradi pamoja na kuishukuru serikali ya Canada kupitia kwa balozi wake hapa nchini Pamela O’Donnel ambayo imetoa fedha za kusaidia ukarabati wa chuo hicho na vyuo vingine 3 vya ualimu nchini.
Sambamba na mradi huo Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali inatekeleza miradi mingine ya elimu mkoani Mtwara ukiwamo mradi wa ukarabati shule 3 kongwe za sekondari Mtwara Ufundi, Chidya na Ndwika kwa gharama ya shilingi bilioni 10.9 na kutekeleza sera ya elimu bure ambapo tangu kuanza kwa utekelezaji wake disemba 2015 mkoa umepokea shilingi bilioni 23.02 sawa na wastani wa 8.5% kwa kila mwaka.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Joyce Lazaro Nalichako (Mb) amesema chuo hicho ni chuo kongwe kwani kilianzishwa mwaka 1937 kama middle School chini ya kanisa Katoliki na Mwaka 1975 ndipo kilipoanza rasmi kama Chuo cha Ualimu chini ya usimamizi wa Serikali na ukongwe huo ndio uliopelekea uchakavu wa majengo.
Waziri Ndalichako amesema kuwa mradi huo unatekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushiriana na serikali ya Canada na unahusisha vyuo 4 vikongwe vya ualimu hapa nchini, Chuo cha Ualimu Kitangali, Ndala, Shinyanga na Mpuguso mradi unaogharimu shilingi bilioni 36 na milioni 475, ambapo serikali ya Tanzania imechangia shilingi bilioni 8 na milioni 200 huku serikali Canada ikichangia shilingi bilioni 28 na milioni 275.
Hata hivyo Mhe. Ndalichako amishukuru serikali ya Canada kwa ushirikiano wanaoutoa kwa serikali Tanzania kupitia Wizara ya Elimu kwani majengo ya vyuo hivyo yamebadilika na kuwa ya kisasa na ukarabati huo umehusisha madarasa, mabweni, maabara, kuktaba, uchimbaji wa visima, ofisi, majiko pamoja na kazi za nje “lakini Mhe. Rais katika chuo cha ualimu cha Kitangali mradi huu unaotekelezwa ambao mhe. Rais unakwenda kutuwekea jiwe la msingi unagharimu fedha shilingi bilioni 8 na milioni 269”. Alieleza Waziri Ndalichako.
Naye balozi wa Canada nchini Pamela O’Donnel amesema Serikali ya Canada itaendelea kushirikiana Tanzania katika sekta ya elimu kwani wameridhishwa na usimamizi nzuri wa fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa baina ya nchi hizo mbili na utekelezaji wa mradi huo utaisaidia nchi kutoa waalimu bora 3300 kila mwaka.
Balozi O’Donnel amesema dhamira ya serikali ya Canada ni kuisaidia elimu ya Tanzania hasa wanawake na vijana na kuona usawa wa kijinsia unapatikana, kwani elimu ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na sasa wanaanzisha mradi mwingine ambao tayari umetiwa saini unaogharimu dola za Canada milioni 53 Maradi wa kusapoti elimu ya ualimu (TSP) wenye lengo la kuboresha mbinu za wakufunzi na waalimu wanafunzi kwenye vyuo vya waalimu 35 nchini.
Akiongea katika hafla hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Newala mjini amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Magufuli, na serikali yake kwa ujumla kwa kusikia kilio cha wananewala kwani hatua hiyo inaonyesha dhamira ya dhati ya serikali ya kuwatumikia wananchi wake.
Aidha pia Mhe. Mkuchika ameishukuru wizara ya elimu chini ya usimamizi wa taasisi ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kwa kukubali kuanzisha chuo cha ufundi stadi mwezi julai mwaka huu, baada ya kuwapatia majengo ya iliyokuwa sekondari ya Newala Development Fund (NDF) eneo la mji mdogo wa Kitangali.
Kuhusu korosho Mhe. Rais Magufuli amesema hajaridhishwa kuona baadhi ya viwanda vya kubangua korosho vilivyoanzishwa na Baba wa Taifa mkoani hapa vikiwa havifanyi kazi hivyo ameiagiza wizara ya wiwanda na viongozi wa mkoa kukaa pamoja na kutafuta njia ya kuvifufua viwanda hivyo.
Hata hivyo ameeleza kuwa wakulima halali waliouza korosho ambao hawajapata malipo yao, wasiwe na wasiwasi seriakali haijafunga msimu na tayari imatoa shilingi bilioni 50 ambazo kuanzia sasa muda wowote zitaanza kuinginzwa kwa wakulima huku akisisitiza walionunua kangomba kama wanataka kulipwa ni lazima waandike baurua za kukiri kufanya hivyo na halamashauri zisahau juu ya kupata ushuru wa mauzo hayo.
Raisi Magufuli yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu iliyoanza juzi Jumanne tarehe 02 Aprili, 2019 ambapo alikuwa Mtwara mjini kaweka jiwe la msingi mradi wa upamuzi uwanja wa ndege na kubangua kiwanda cha kubangua Korosho cha YALIN, jana jumatano tarehe 03 April, 2019 aliweka jiwe la msingi maradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 50 eneo la Naliendele barabara ya Mtwara – Mnivata na kuweka jiwe la msingi mradi wa ukarabati na upanuzi wa chuo cha ualimu kitangali Newala.
Aidha jana akiwa katika ziara hiyo Mhe. Rais aliiagiza wizara ya ujenzi kutangaza tenda ya ujenzi wa kilomita 100 za barabara kutoka Mnivata mpaka Newala kwa kiwango cha lami na leo atahitimisha ziara yake kwa kuzitembelea wilaya za Masasi na Nanyumbu.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa