Baraza la madiwani la halmashauri ya mji ya Newala, limezinduliwa rasmi jana tarehe 03 disemba, 2020 huku madiwani wateule wakitakiwa kuwasilisha hoja za maendeleo ya wananchi badala ya hoja zao binafsi.
Hayo yameeleezwa na mgeni rasmi katika kikao hicho cha uzinduzi, Katibu tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alphayo Kidata wakati wa hotuba yake ambapo amesema wao ni wawakalishi wa wananchi hivyo jukumu lao kubwa ni kusimamia maslahi ya wananchi waliowachagua.
Aidha amesema sambamba na jukumu hilo ni wajibu wao kusimamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kwa kuwa ndilo jawabu la kufanikisha utekeleaji wa miradi ya maendeleo na kutimiza ahadi walizoweka na wananchi wakati wa kuomba kura.
Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Yusuph Kateule amewataka madiwani kuwa na uvumilivu katika utendaji wao wa kazi kwa kujitume ili wananchi waliowachagua wanufaike matuma ya kile walichokipanda kwenye masanduku ya kura.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Newala amewaomba madiwani kutambua miradi ya maendeleo ni ya wananchi wenyewe, hivyo wanatakiwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza katika utekelezaji wa miradi itakayo jitokeza pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na watendaji wa seriakali.
Naye Mbunge wa jimbo la Newala Mjini Kapteni Mstahafu Mhe. George Mkuchika amelitaka baraza hilo kuhakikisha linaweka kipaumbele kwenye masuala ya afya kwa kusimamia ujenzi wa vyoo bora na usafi wa mazingira unaoenda sambamba na ukuaji wa mji wa Newala.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amewataka madiwani wanawake wawe wajenga hoja za kutetea maslahi ya wanawake na wananchi waliowachagua ili kuonyesha thamani ya mwamamke kwenye jamii katika kuelekea ajenda ya 50 kwa 50.
Baraza hilo lenye jumla ya madiwani 20 wa CCM na mmoja CUF lilizinduliwa kwa kuanza kuwaapishwa madiwani wote, kuchangua mwenyekiti ambaye ni Mhe. Yusuph Halfani Kateule na makamo wake Mhe. Hamisi J. Namata wote kutoka CCM pamoja na kuunda kamati mbalimbali za kudumu za halmashauri.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa