Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanazani, imetenga shilingi bilioni 1.6 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuboresha wa huduma katika sekta afya ndani ya Halmashauri ya Mji Newala.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wanawake Taifa Bi. Subira Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum mkoani Pwani anayewakilisha wanawake (CCM) wakati wa ziara ya viongozi wa Jumuiya hiyo wilayani Newala kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Bi. Mgalu akiongea na wananchi wa kata ya Nanguruwe kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo amesema serikali kupitia bunge la bajeti limetenga shilingi milioni 900 kufanya maboresho kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Mji Newala ambayo ni kongwe.
Aidha ameongeza kuwa kwenye sekta ya afya halmashauri ya Mji Newala imetengewa fedha shilingi milioni 600 kununua vifaa tiba kwenye vituo vya afya vilivyokamilika pamoja na shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukunua vifaa tiba kwenye zahanati.
“Tumetoka kwenye bunge la bajeti mambo yenu Newala yako supaa… kwenye sekta ya afya nimeona uzuri wa majengo yale lakini ukweli vifaa tiba badooo… Mheshimiwa Rais amewatengea fedha ya kutosha katika sekta ya afya ndugu zangu haya ninayoyasema sio Newala pekeyake ni Tanzania nzima”. Alifafanua mjumbe huyo.
Sambamba na hilo ziara hiyo imebeba ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto ambapo jamii imetakiwa kuwa mlinzi wa usalama wa mtoto huku wananwake wakitakiwa kuwa mstari wa mbele kwa wao ndio wamebeba hatma yao kupitia malezi na ukuzi.
Akisoma taarifa ya Halmashauri mbele ya kiongozi huyo Mtakwimu wa halmashauri Ndg. Simplis Frank amesema halmashauri wanaishukuru serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kuwaletea wataalam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa halmashauri inaendelea kutekeleza ilani ya CCM ya 2020-2025 ibara ya 80D ambapo kwa miaka mitatu wameongeza vituo vya afya vinavyotoa huduma kutoka kimoja mpaka vitatu na kwamba halmashauri imepokea shilingi bilioni 1.59 kutoka serikali kuu.
“Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya na ununuzi wa vifaa tiba kwenye vituo viwili vya Nambunga ambacho tayari kimeanza kutoa huduma na kituo cha Nanguruwe ambacho kimefikia 90% ya ukamilishaji wake”. ilifafanua taarifa hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Kateule ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nanguruwe amesema toka Mheshimiwa Rais Dkt. Samia aingie madarakani kata yake imepokea shilingi bioni 2.8 fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kiwamo ruzuku mashuleni pamoja na wanufaika wa TASAF.
Hata hivyo Mhe. Kateule ameongeza kuwa wananchi wa kata yake wamefurahishwa na kuahidi kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo kutoka na kuwawezesha kujenga kituo cha Afya na ujenzi wa bweni, bwalo na madarasa katika shule ya sekondari Malocho ambayo inatarajia kuanza kidato cha tano kwa wavulana mwezi Agosti mwaka huu.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa