Serikali imewatoa hofu wakulima wa korosho kuwa watalipwa fedha zao muda mfupi ujao huku ikiweka wazi tayari imeshatoa fedha zote za malipo na kilichobaki ni kukamilisha taratibu za uhakiki kwa baadhi ya wakulima na zoezi hilo linatarajia kukamilika ndani ya mwezi wa pili.
Hayo wameelezwa jumamosi 26th,01,2019 na Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Omary Mgunda, wakati anazungumza na wananchi wa kijiji cha Moneka kilichopo kata ya Mtonya ndani ya halmashauri ya Newala akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Newala.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba
Mhe. Mgunda amekiri uwepo wa kuchelewa kulipa wakulima kutokana na changaomoto iliyojitokeza ya kuwa na mnunuzi mmoja ambaye ni serikali baada ya wanunuzi kugomea kununua korosho kwa maslahi ya mkulima, kuchelewa kuanza msimu wa ununuzi na ugeni wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko baada ya kufanyiwa mabadiliko.
Aidha ameeeleza kuwa kumekuwa upotoshwaji wa taarifa unaotokana na kukosekana na uwazi wa taarifa za nani amelipwa na nani hajalipwa kwani hadi sasa kiasi cha shilingi bil. 48 kati ya bil. 61 zimelipwa kwa wakulima wilayani Newala na ameagiza kuanzia sasa majina yote ya wakuliwa waliolipwa yawekwe kwenye mbao za matangazo.
Awali akisoma taarifa ya zao la korosho Mkuu wa Wilaya Newala Mhe. Aziza Mngosongo amesema kwa msimu wa mauzo wa 2018/2019 jumla ya tani 20,969.160 za korosho zimeuzwa kutoka kwa wakulima 64,905 wilayani hapa na wakulima hao 58,569 kati yao wameshafanyiwa uhakiki na 6,336 wanaendelea na zoezi la uhakiki , huku tani 19,910.231 zimeshahakikiwa.
Akiongea kwa niaba ya wakulima wa korosho Nchini, Bwana, Jafari Hakika Mbota amempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa hatua aliyoichukua ya kuwakomboa wakulima kwa kununua korosho, lakini amewataka wasimamizi wa malipo wasimtie doa Mhe. Rais kwa kuchelewesha malipo kwani wakulima wapo kwenye hali mbaya ya kiuchumi na kwa wale ambao hawalipwa upo uwezekano mkubwa wa kushindwa kufanya maandalizi ya kilimo katika kipindi kinachoendelea cha masika.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa